Na Walter Mguluchuma -Katavi
Kampuni ya ununuzi wa zao la Tumbaku ya PREMIUM ACTIVE TANZANIA LIMITED limekabidhi msaada wa
madawati 136 kwa Halmashauri ya
Wilaya ya Mlele yatakayo saidia kupunguza
tatizo la wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini ikiwa ni sehemu ya
Kampuni hiyo kurudisha
sehemu ya faida yake kwa jamii kuchangia maendeleo .
Muonekano wa Madawati 1000 yaliyotolewa na Kampuni ya PREMIUM ACTIVE TANZANIA Mkoa wa Katavi kwenye maeneo yanayolima zao la Tumbaku ikiwa ni sehemu ya faida wanayoipata kurudisha kwenye jamii.. |
Kampuni ya ununuzi wa zao la Tumbaku ya PREMIUM ACTIVE TANZANIA LIMITED limekabidhi msaada wa madawati 136 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele yatakayo saidia kupunguza tatizo la wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini ikiwa ni sehemu ya Kampuni hiyo kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii kuchangia maendeleo .
Roussos amesema lengo la utoaji wa mchango huo
wa Kampini ya PREMIUM ni
kurudisha sehemu ya
faida wanayopata kwa maendeleo
ya jamii katika maeneo ambayo wanafanya
shughuli za ununuzi wa zao la Tumbaku .
Nicco Roussos Meneja Shughuli kutoka Kampuni ya PREMIUM ACTIVE TANZANIA akielezea namna Kampuni hiyo inavyo shirikiana na serikali kuinua elimu kupitia zao la Tumbaku. |
Kwa kuzingatia uzalishaji
wa msimu wa kilimo 2024
Kampun imeweza kutoa kiasi hicho cha madawati
136kwa Halmashauri hiyo ya Mlele
yenye thamani ya tshs 9,520,000 kati ya madawati 1000 yatakayo gawa kwenye maeneo wanayonua tumbaku ya Wilaya za
Tanganyika ,Mpanda , Chunya , Songwe
yatakayo tumia kiasi cha Tshs
71.070,000.
Amevitaja vijiji ambavyo vimenufaika katika Halmashauri hiyo kuwa ni Wachawaseme wamepata dawati 34,Mgombe dawati 34,Kamsisi
34 na Inyonga 34.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Igombe Halmashauri ya Wilaya ya Mlele wakiwa darasani waliopatiwa msaada wa Madawati na Kampuni ya PREMIUM ACTVE TANZANIA. |
Roussos
amesema utoaji wa vifaa
hivyo unazingatia maombi ya
wanufaika pamoja na fedha
inayokuwa imetengwa kutokana na uzalishaji wa wilaya husika
au kata husika
hivyo wanaendekea kusisitiza uzalishaji
bora wa wakulima ambao utakuwa na tija kwa jamii na wakulima pia
wanasihi wakulima waendelee
kutunza mazingira kwa kupanda miti na kuboresha majiko yanayotumia kuni kidogo
za matawi.
Meneja shughuli na Mhusiano wa Kampuni ya Premium Yusuph Mahundi
amesema msaada huo waliootowa ni
sehemu ya kampuni yao katika kuisaidia Serikali kwenye maswala ya kuisadia Serikali kwenye maswala ya maendeleo ya jamii .
Ameeleza kuwa kwenye Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Mlele kampuni hiyo inafanya kazi na vyama vitatu vya Msingi katika ya vyama 50 wanavyofanya navyo kazi hapa nchini pia pamoja na madawati hayo pia wanatowa ushuru kwenye Halmashauri katika maeneo yote wanayonunua tumbaku ambazo ni zaidi ya Dola 107 000 na kwa Mkoa wa Katavi wanalipa zaidi ya Dola 6,000 kwenye halmashauri zinazolima Tumbaku .
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Beatrice Rumbeli amesema msaada huo wameopokea kwa mikono miwili na wataendelea kuiinga mkono kampuni hiyo kwa jitihada zake kubwa za
kutunza mazingita
Kaimu katibu
Tawala wa Wilaya ya Mlele Geofey
Uwahanja amesema tatizo la upungufu wa madawati lipo karibu kwenye maeneo ya Halmashauri zote
mbili za Wilaya hiyo hivyo Kampuni hiyo isisite tena kutowa msaada kama huo.
Kaimu afisa elimu elimu ya
Msingi wa Wilaya ya Mlele Peter Nyamafu
ameeleza kuwa kampuni isiwachoke
kwani Halmashauri hiyo inaupungufu
wa madawati 4524 hivyo upingufu bado ni
mkubwa hivyo wanawaomba wawaongezee
tena ili
wawaweze kupunguza upungufu uliopo .
Amesema vilevile wanaonba wasaidiwe vitu vingine kwani kwenye swala la elimu bado kuna vitu vingine vinahitajika kama vile madarasa na matundu ya vyoo.