TAKUKURU KATAVI WAOKOA ZAIDI YA MILIONI 90 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU

Stewart Kiondo Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi akisoma repoti ya utendaji kazi ya kipindi cha miezi mitatu kuanzia Oktoba mwaka jana hadi mwezi Desemba 2024.

Na  Walter Mguluchuma, Katavi 

Taasisi ya  Kuzuia  na Kipambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi  imefanikiwa  kuokoa  kiasi cha zaidi ya shilingi   Milioni 90 za  chama  cha  Msingi  Ilangu cha Wakulima wa Tumbaku Wilaya  ya Tanganyika  Mkoani  Katavi .

Naibu  Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi  Stewart  Kiondo amewaambia  wandishi wa  Habari wabari  wakati alipokuwa akitowa taarifa ya  utendaji kazi ya  kipindi cha miezi mitatu ya  kuanzia  Oktoba mwaka jana hadi mwezi Desemba.

Amesema  Takukuru Mkoa wa Katavi  katika  majukumu  yake  katika eneo la  uzuiaji wa  Rushwa  na ufatiliaji wa miradi  ya Maendeleo  imefanikiwa  kuokoa  kiasi  cha  Tshs  91,000,000 za  chama  cha Msingi  Ilangu  AMCOS  kilichopo katika Wilaya ya Tanganyika .

Amebainisha  kuwa  Takukuru Mkoa wa Katavi  walipata  malalamiko  juu ya  ubadhilifu  wa mbolea  aina ya NPK    katika  chama cha  Msingi cha wakulima wa Tumbaku  Ilangu  kinachoshirikiana  na  chama kikuu cha  LATCU  katika kufanya shughuli  zake  za ushrika ,

Kiondo amesema   kwenye  Amcos  walitakiwa  kupokea   mifuko ya mbolea  9500 lakini waliweza kupokea mifuko 8879  kukiwa na upungufu wa mifuko  621 ya  mbolea ya Npk inayotumika kwenye zao la Tumbaku  yenye thamani ya  tshs  91,000,000 ilichukuliwa na viongozi wa AMCOS ya Ilangu  kwa kushirikiana na mtumishi mmoja asiye mwaminifu wa LATCU .

Baaada ya ufatiliaji  wa  Takukuru waliweza kubaini  kuwa  kampuni  ya NGESACO  SERVICE  LIMETED  ndio waliolipwa fedha hizo  na  kufuatia  kubainika  kwa kampuni hiyo kulipwa fedha hizo ambazo hawakusitahili  waliwataka warudishe fedha hizo.

Ndipo kampuni  hiyo ilipoweza kurejesha kiasi cha  tshs 59,150,000 ambapo mwenyekiti wa Ilangu Amcos  nae aliweza kurejesha kiasi cha Tshs  31,850,000 kwa Takukuru  zikiwa  ni  fedha za Ilangu  Amcos   na kufanya  fedha zilizo okolewa kuwa ni tshs  91 000,000 licha ya  kurudishwa  fedha hizo Takukuru  bado wanaendelea na  uchunguzi wa fedha hizo  ambazo  zilikuwa zikichepushwa kwa manufaa binafsi .

Kiondo amesema   katika kipindi  hicho wameweza  kufatilia miradi  27 yenye  thamani ya  Bilioni  7.6 katika sekta za  elimu   afya , ulinzi  na  usalama  na  maendeleo ya  jamii katika  miradi hiyo  kuna  baadhi  wamebaini inachangamoto  ambayo imesababisha miradi kukamilika kwa wakati .

Hivyo  Takukuru wanaendelea kufanya uchunguzi  juu    ya  hayo waliyoyabaini  kwenye miradi hiyo  ikiwa ni  kuwepo   na  manunuzi hewa  ya  thamani  madawati 50 pamoja  na  matofali  yenye  ubora  kwenye baadhi ya shule za  msingi  zenye  miradi  hiyo .


Kuhusu  malalamiko ya Rushwa wameweza kupokea jumla ya malalamiko  34 kati  ya  malalamiko  hayo  taarifa za  rushwa zilikuwa ni  21  na  zisizo za  rushwa  ni   13 na yalihusisha sekta  za uhamiaji , Serikali za  mitaa , ardhi , biashara maliasili na Polisi .

Aidha  Takukuru  Mkoa wa Katavi wamewakunbusha wananchi wa mkoa  huu kuendelea kutowa taarifa za vitendo vya Rushwa pindi wanapokuwa wameona  vinapokuwa  vinataka kutokea au kutokea kwa  kutowa taarifa kwenye Taasisi hiyo ili waweze kuchukua hatua kwa  haraka.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages