Nicco Russos [kulia]Meneja wa Shuguli kutoka PREMIUM ACTIVE TANZANIA akimkabidhi Madawati Lincolin Tamba [kushoto] Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Uongozi
wa Serikali ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wameyaomba Makampuni ya
ununuzi wa zao la Tumbaku kuiga mfano wa Kampuni ya PREMIUM ACTIVE TANZANIA ya
kurudisha sehemu ya faida yao kwenye Jamii kwaajili ya kuchangia maendeleo kama
inavyofanya Kampuni hiyo.
Uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wameyaomba Makampuni ya ununuzi wa zao la Tumbaku kuiga mfano wa Kampuni ya PREMIUM ACTIVE TANZANIA ya kurudisha sehemu ya faida yao kwenye Jamii kwaajili ya kuchangia maendeleo kama inavyofanya Kampuni hiyo.
Wito
huo umetolewa na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Lincolin Tamba
ambae ni Katibu tawala wa Wilaya hiyo ya Tanganyika aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya kwenye hafla
ya kukabidhiwa Madawati 456 kutoka Kampuni ya PREMIUM ACTIVE TANZANIA kwaajili
ya Halmashauri ya Wilaya hiyokwenye maeneo wanayolima zao la Tumbaku.
Amesema
kuwa Wilaya hiyo imepokea Madawati 456 kutoka Kampuni ya PREMIUM ACTIVE
TANZANIA ikiwa ni sehemu ya kurudisha sehemu ya faida yao kwenye Jamii kwaajili
ya kuchangia maemdeleo hususani kwenye sekta ya Elimu.
Lincolin Tamba Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika ambae pia ni Katibu Tawala Wilaya ya Tanganyika akitoa neno la Shukrani kwa Kampuni ya PREMIUM ACTIVE TANZANIA kwa msaada wa Madawati 456. |
Amesema Vijiji vitakavyo nufaika na Madawati hayo nipamoja na kijiji cha Isubangala,Busongola,Majalila,Isenga,Lugufu,Isungwe,Kabanga,Kamjela,Igagala,na Kabungu ambavyo kwa sehemu kubwa vinajihusisha na kilimo cha zao la Tumbaku.
Amesema
kuwa Tumbaku inayozalishwa katika Wilaya ya Tanganyika kwa asilimia tisini
imekuwa ikinunuliwa na Kampuni ya PREMIUM ACTIVE TANZANIA na ndio wanunuzi
wakubwa wa zao hilo kwenye wilaya hiyo kwani katika vyama Tisa vya Msingi
vinavyozalisha zao la Tumbaku imeonekana kampuni hiyo hufanya kazi na vyama 8
vya Msingi namatokeo yake yanaonekana kwa kupatiwa Madawati hayo 456.
Amemshukuru
Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutengeneza mazingira wezeshi kwa Kampuni ya
PREMIUM ACTIVE TANZANIA kufanya shughuli
zake katika Wilaya hiyo bila kikwazo cha aina yeyote.
Amesema
Halimashauri hiyo inaupungufu mkubwa wa Madawati hivyo Madawati hayo 456
yatakwenda kupunguza tatizo la uhaba wa Madawati kwa kaiasi frani yatakwenda
kupunguza uhaba huo na hawajapokea Madawati tu bali wamepokea madawati mazuri
na yenye ubora yaliyotengenezwa kwa kiwango.
Hivyo
ameomba Makampuni mengine ya ununuzi wa Tumbaku kuiga mfano mzuri ulionyeshwa
na kampuni ya PREMIUM ACTIVE TANZANIA kwa kutoa msaada huo wa Madawati 456
kupitia sehemu ya faida .
Kwa
upande wake Nicco Russos Meneja wa Shughuli Kutoka PREMIUM ACTIVE TANZANIA
amesema kuwa mwaka huu 2025 Kampuni hiyo imetoa Madawati 456 ambayo yanathamani
ya shilingi Milioni 31920,000 kwa Wilaya ya Tanganyika kwa mkoa mzima wa Katavi
wametoa Madawati 1000 yenye Thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 71.
Russos
amewasihi wakulima kuendelea kupanda miti kwaajili ya kuboresha mazingira na
kutumia yanayotumia kuni kidogo kwaajili ya kukaushia zao la Tumbaku.
Meneja
shughuli na mahusiano Yusuph Mahundi
amesema katika Wilaya ya Tanganyika kwa msimu uliopita walifanya kazi na vyama
vya Msingi 9 kwa msimu huu wanafanya kazi na vyama vya msingi 8 kati ya vyama
50 vya msingi wanavyofanya navyokazi hapa nchini.
Mahundi
amesema kuwa kwenye eneo la ulipaji wa ushuru mwaka huu Kampuni hiyo imelipa
zaidi ya Dola 342000 za kimarekani kati ya Dola zaidi ya Laki sita zinazolipwa
kwa Mkoa wa Katavi.
Amewahakikishia
Wakulima wa zao la Tumbaku kwa Mkoa wa Katavi kuwa sehemu hiyo waliyoitoa
wataendelea kutoa kila mwaka kama ambavyo wamefanya mwaka huu.
Ojungu
Sabaya Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika amesema Halmashauri
hiyo inaupungufu wa Madawati 25000 kwa msaada huo waliowapatia niwakipee kwani
utakwenda kupunguza upungufu wa madawati na wameisadia serikali.
Sabaya
ameendelea kuwaomba isiwe mwisho hapo bali wasaidie kwenye miundombinu mingine
kama sera yao inavyosema.
Sadam Juma Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mpanda ndogo amesema wanashukuru kwa msaada huo kutoka Kampuni ya PREMIUM ACTIVE TANZANIA na kuahidi kusoma kwa bidii.