KATAVI KUZINDUA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akitoa taarifa ya uzinduzi wa Kampeini ya Msaada wa Kisheria kwa Mkoa wa Katavi inayojulikana kama Samia Legal Aid Kampeini 

Na Walter Mguluchuma-Katavi

Wananchi wa Mkoa wa Katavi wanatarajia  kunufaika na huduma ya  msaada wa Kisheria  wa Mama Samia (LEGAL AID  KAMPEINI) itakayotolewa  kwenye maeneo ya Halmashauri  zote tano zilzopo katika Mkoa wa Katavi  pasipo malipo ya aina yoyote .


Wananchi wa Mkoa wa Katavi wanatarajia  kunufaika na huduma ya  msaada wa Kisheria  wa Mama Samia (LEGAL AID  KAMPEINI) itakayotolewa  kwenye maeneo ya Halmashauri  zote tano zilzopo katika Mkoa wa Katavi  pasipo malipo ya aina yoyote 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko  amesema  uzinduzi wa   huduma  hizo za  msaada wa kisheria  utafanyika Januari  24 katika uwanja wa shule  ya msingi Kashaulili  uliopo katika Manispaa ya  Mpanda .

Amebainisha kuwa kampeni   hiyo ya Mama  Samia itafanyika kwa muda wa siku  kumi  siku  hiyo ya tarehe 24 itakuwa ni siku ya uzinduzi na baada ya hapo  kazi  itafanyika katika maeneo yote ya Halmashauri za Mkoa wa Katavi.  

Lengo  la Kampeni hii  ambayo Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan ameridhia ifanyike ni pamoja  na kuhakikisha kwamba wananchi wasio na uwelewa wa kisheria  wanapata  uelewa kuhusu mambo ya kisheria  na pia itahusika na utatuzi wa  changamoto mbalinbali za  kisheria  ambazo wananchi watakuwa wanaziwasilisha  kwenye timu za wanasheria  wasaidizi watakao kuwa wanafanya kazi hiyo ,

Mrindoko amesema kampeni hiyo itakuja kutowa msaada wa kisheria  kwa wananchi ndani ya Mkoa wa Katavi  na kuwafanya wananchi waweze kupata haki zao za msingi za kisheria   kwa kufuata  maelekezo na taratibu .

Amefafanua kuwa  kampeni hii inakauli mbiu  inayosema MSAADA  WA  SHERIA  KWA  HAKI USAWA  AMANI  NA MAENDELEO na  kauli mbiu hii inaashiria  kulinda   na kutetea haki za wanyonge  na kupinga uvunjaji wa haki za Binadamu  na kuelewesha   wananchi misingi ya   utawala bora na kupinga ujatili wa kijinsia  pamoja na kuendelea  kuwaelimisha wananchi kutii sheria na ueawala bora .

Mkuu wa Mkoa  Mrindoko amemshukuru Rais Samia kwa  kuridhia  kufanyika kwa kampeni hii katika Mkoa wa Katavi  ambapo kwenye kila Halmashauri itafanyika kwenye Kata kumi  na  vijiji kumi kwenye kila Halmashauri  kwa maana hiyo kwa Mkoa huu itafanyika kwenye Kata 45, mitaa 26 na vijiji 114 kwa  mkoa mzima wa Katavi

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages