Naibu waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya alipotembelea Mradi wa ujenzi wa Daraja la Mirumba Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi. |
Naibu Waziri wa
ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amewakata wakandarasi
wote nchini wanaopewa kufanya kazi za miradi mikubwa na midogo
kuitekeleza kwa ubora na kwa wakati ili waweze kuaniniwa
Naibu waziri wa ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya [katikakati] akigagua mradi wa ujenzi wa Daraja la Mirumba[kulia] ni Meneja wa Tanrods Mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende
Naibu Waziri wa ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amewakata wakandarasi wote nchini wanaopewa kufanya kazi za miradi mikubwa na midogo kuitekeleza kwa ubora na kwa wakati ili waweze kuaniniwa
Maelekezo hayo
kwa Wakandarasi ameyatoa wakati akikagua
ujenzi wa daraja la Mirumba Wilayani Mlele
linalounganisha mikoa ya Katavi na Rukwa linalojengwa kwa gharama ya zaidi ya
Bilioni 6.3 ujenzi unaofanywa na mkandarasi mzawa kampuni ya M/ s
Safari General Business Co Ltd JV Mbuya Contractors Co
Ltd kwa usimazi wa Taroads Katavi .
Amesema mradi huo unaojengwa kwa fedha za kutoka Benki ya Dunia ni miongoni
mwa miradi mitatu inayotekelezwa katika Mkoa wa Katavi kwa kipindi
cha miezi 12 na itagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 17.2 ambapo
kwa daraja la Mirunba litatumia zaidi ya Bilioni 6.3.
Amesisitiza kuwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan ameekeza kuwawezesha wakandarasi wazawa hivyo miradi wanayokuwa wanepewa kufanya kazi wazawa watambue wanapofanya vizuri ndio inakuwa ni kipimo chao cha kuwafanya wazidi kuaminiwa.
amewaomba wakanadarasi hao miradi wa wanayokuwa wanapewa wanapaswa kuifanya kwa ubora na
kwa wakati iliwawe kuonyesha wanaweza kupewa kazi wazawa.
Amefafanua kuwa
ilikuonyesha kuwa wanaweza ni vema wakaonyesha wanaweza
kufanya kazi ya miradi mikubwa kwa ubora na kwa
wakati .
Mhandisi Kasekenya amesema lengo la Rais anataka wakandarasi wazawa wakuwe na fedha zetu zibaki hapa nchini kuliko kumpatia mkandarasi wa kigeni ambae akilipwa fedha hiyo hupeleka nchini kwake.
Ni jukumu sasa kwa wakandarasi zawa kumwakikishia Rais kuwa wanaweza kwa kufanya kazi zenye ubora.
Na
wameisha kubaliana mawaziri wa fedha na Ujenzi kutoa nafasi
kwa wazawa kufanya kazi ya miradi mpaka inayofikia Bilioni 50 ijengwe na
wazawa Watanzania
Kwa miradi inayotekelezwa sasa itatoa mwelekeo kwa serikali namna wanavyotekeleza miradi hiyo na serikali haipo tayari kupoteza fedha kwa kuona miradi inajegwa chini ya kiwango.
Amesema ili waendelea kwenda mbele ni wao kuonyesha Serikali ilivyowaamini waonyeshe kuwa wanaweza kwa kutekeleza miradi inavyotakiwa na wala si vinginevyo kwani Rais ana Imani nao na ndio maana amasema miradi mikubwa wapewe wazawa .
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende ameeleza kuwa wamefanikiwa kupata miradi 3 ya ujenzi wa madaraja yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 17.2
Miradi hiyo
yote mikubwa mitatu inatekelezwa na wakandarasi wote wazawa na
itatekelezwa kwa kipindi cha miezi 12 na tayari imeanza utekelezaji wake katika
hatua mbalimbali .
Mhandisi Mwakabende ameitaja miradi hiyo mitatu inayofadhiliwa na Benki ya Dunia kuwa ni ujenzi wa daraja la Sitalike linalounganisha Mkoa wa Katavi na Rukwa.
Na Daraja la Mirumba na madaraja madogo 16 ya kutoka Maji Moto hadi Kilida