UZINDUZI WA SAMIA LEGAL AID KAMPEINI WAFANA KATAVI

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akiwahutibia wananchi wa Mkoa wa Katavi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria inayojulikana kama Samia Legal Aid Campeing

Na Walter Mguluchuma-Katavi

Mkoa wa Katavi  umezindua  kampeni ya siku kumi ya msaada wa kisheria wa Mama Samia inayotekelezwa  Tanzania Bara na Zamzibar  yenye lengo ya kulinda, kukuza na upatikanaji  wa haki kwa watu wote   kupitia huduma  ya msaada wa kisheria  hapa  Nchini .


Mkoa wa Katavi  umezindua  kampeni ya siku kumi ya msaada wa kisheria wa Mama Samia(MSLG) inayotekelezwa  Tanzania Bara na Zamzibar  yenye lengo ya kulinda, kukuza na upatikanaji  wa haki kwa watu wote   kupitia huduma  ya msaada wa kisheria  hapa  Nchini .

Uzinduzi  huo umefanyika  katika  uwanja wa  shule ya Msingi  Kashaulili na umezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko  na huduma hiyo  itatolewa na wanasheria wa kutoka  Wizara ya sheria na Katiba ,wanasheria wa Halmashauri   mawakili wa kujitegemea  na wasaidizi wa kisheria .

Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba  Franklin  Rwezumula  amewaambia wananchi wa Mkoa wa Katavi na Watanzania  kwa ujumla wakati wa  uzinduzi huo kuwa  Wizara ya Katiba  na sheria inatekeleza kampeni hiyo kwa mujibu wa  ibara ya 13 ya  katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   inayotamka usawa mbele ya sheria   na utekelezaji wa msaada wa kisheria  yam waka 2017 ambapo inatowa  mwongozo wa utoaji wa msaada wa kisheria  kwa wananchi wote wasiokuwa na uwezo .

Amee;eza  uzinduzi wa  kampeni hii  ilizinduliwa na  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Kassimu  Majaliwa   mwaka 2023 Mkoani  Dodoma  na utekelezaji wa kampeni hii  sasa umefika katika mikoa 11 na  kwenye  kampeni  kama hiyo ilizinduliwa  Mkoani  Katavi itazinduliwa  katika mikoa sita na kufanya mikoa itakayokuwa imefikiwa kuwa 17

Utekelezaji wa Kampeni hiyo unaenda  sambamba  na utoaji  wa elimu wa Uraia  na utawala bora kwa viongozi  wa ngazi mbalimbali  wakiwemo wajumbe wa kamati za usalama za Mikoa  wilaya wakuu wa vitengo  vya  vivisheni wa mikoa  na Wilaya na watendaji wote wa  Kata wa Mikoa  yote  ambayo itafikiwa na kampeni .

Rwezumula  amebainisha kuwa  malengo ya mkakati huu ni pamoja na  kuwajengea uwezo  washiriki   kuhusu haki na wajibu wao  kikatiba  na  kuwaongezea uwelewa washiriki  kwenye maswala ya uraia , haki za binadamu  misingi ya utawala bora na demokrasia  na  katika kuhakikisha   kuwa  uendelevu  wa  huduma za msaada wa kisheria  Wizara imeanzisha madawati ya msaada  wa  kisheria katika Halmashauri zote   nchini .

Amesema  madawati  hayo  kwa kushirikiana  na  mashirika  ya utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria  na wasaidizi wa kisheria chini  ya  wasajiri wasaidizi  ngazi ya Mkoa  na Halmashauri  yataendelea kutowa huduma   hata baada ya kumalizika kwa kampeni hiyo  amemwomba mkuu wa Mkoa kuendelea kuwapa ushirikiano  ili waweze kuwafikia wananchi kwa wakati .

Baada ya uzinduzi huo kampeni hiyo kwa Mkoa wa Katavi itaendelea hadi   tarehe   mbili mwezi wa pili 2025 na lengo la Wizara ya Katiba na sheria ni kuzifikia Halmashauri zote  na kila  halmashauri watazifikia kata kumi   na kila   kata watafikia   vijiji au mitaa mitatu  na timu za wataalamu zitafika pia kwenye shule za msingi  na   sekondari na kutowa elimu  ya  maswala ya  ukatili wa kijinsia  haki  na wajibu wa wanafunzi .

Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Mwanamvua Mrindoko amesema  ni  muhimu kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi  kusimamia  kampeni hiyo kwa  ukamilifu ili wananchi waweze kujitokeza kwa wingi na kuweza kupatiwa msaada huo  muhimu wa kisheria .

Mrindoko amesema    vema kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi wakatumia  vizuri  nafasi hiyo ya  kampeni ya msaada wa kisheria  ili kuwa na  uwelewa mpana zaidi katika  maswala yanayohusu sheria  na kuweza kutetea haki zao za  msingi  na kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu  na pia kuimalisha  maswala ya utawala bora .

Amasema kama ambavyo Wanzania wanavyofahamu  Rais  Samia  Suluhu Hassan  adhima yake ya kukuza  na kutetea  wanyonge na kupinga  uvunjaji wa haki za binadamu  na pia kuimarisha  misingi ya utawala bora  kuepukana na kuelimika  kutokana na  maswala ya kijinsia  na kuimiza kuheshimu  sheria na utawala  katika ngazi zote  na kwa kila mwanamchi  wa Tanzania .

Ameeleza kuwa Rais  amekuja na kampeni  yake ya R4  ambayo inahusisha  maridhiano  usitahimilivu  mageuzi  pamoja na kujenga  upya  misingi ya  sheria na utawala bora  na haki za  binadamu  katika nchi yetu  ya Tanzania  hivyo  ni vema   msaada huu wa kisheria  ukawafikia wananchi  kwa kupata elimu inayohusiana na sheria .

Mjumbe wa  kamati ya  kudumu  ya Bunge  utawala Katiba na Sheria  Boniface Butondo  ameushukuru  uongozi wa Mkoa wa Katavi kwa jinsi walivyojipanga vizuri na kuhakikisha kampeni hiyo  ya msaada wa kisheria  kisheria inafanikiwa vizuri kutokana na maandalizi yao  mazuri waliofanya .

Amesema  pamoja na jitihada za  maendeleo zinazofanywa na Rais Samia  maendeleo yamekwenda yamefika kila mtaa na kijiji lakini  Rais  akasema  hapana  jambo la kisheria ni la  msingi sana ndio maana   akaona  ni lazima kuanza jitihada kubwa sana  za  kuhakisha umma  wa Watanzania  wanaanza kupata elimu na ufahamu  juu ya   mswala mbalimbali ili waweze kuwa na haki  ya kutetea haki zao za msingi

Salome  John Mkazi wa  Manispaa ya Mpanda ameishukuru  Serikali  kwa kuona umuhimu wa kuwaletea  huduma  hiyo  muhimu  mpaka kwenye maeneo ya  kwenye mitaa na kwenye vijiji,

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages