Balozi Mwanaid Maajar Kamishina wa Kamisheni ya Tume ya Rais ya maboresho ya kodi akitoa maelezo mafupi namna ambavyo Tume inavyo sikiliza kero na maoni juu ya maboresho ya kodi. |
Na Walter Mguluchuma, Katavi
Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi imekutana na wafanya bishara na wadau mbalimbali wa Mkoa wa Katavi na kupokea kero mbalimbali zinazo wahusu wafanya biashara na ushauri wa njia bora ya ikusanyaji wa mapato yatokanayo na kodi .
Kikao hicho kilichowashirkisha wadau hao wa Mkoa wa Katavi kilifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na kiliongozwa na Balozi Mwanaid Maajar Kamishina wa Kamisheni wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi ambapo mgeni rasmi kwenye kikao hicho alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa ambae ni Mkuu wawilaya ya Tanganyika Onesimo Buswelu akifungua kikao cha tume ya Rais ya Maboresho ya kodi kilicho washirikisha wafanyabiashara na wadau mbalimbali |
Akizungumza na wadau hao Balozi
Maajar amesema kumekuwepo malalaniko mengi kwa walipa
kodi kuhusu kero zinatokazo na mfumo wa walipa kodi
wanaodai kuwepo kwa utitili wa tozo mbambali na taasisi zinazokusanya kodi .
Amebainisha kuwa kwa hapa nchini
mchango wa ukusanyaji wa kodi upo
chini sana ukilinganisha na nchi za Afrika Mashariki kwa kuona
hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan akaona
ni vyema kuunda tume yenye Makashina tisa ili
kuweza kuwafikia wafanya
biashara katika maeneo mbalimbali
hapa nchini .
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu ameiomba Tume hiyo ya Rais ya Maboresho ya Kodi ichukue
kero na mapendekezo yalitolewa na
wafanya biashara na wadau wengine
walioshiriki kwenye kukao hicho na
kuzifikisha kwa Rais ili ziwezekufanyiwa
utatuzi.
Baadhi ya washiriki wa kikao cha tume ya Rais ya maboresho ya kodi na wafanyabishara na wadau wakifuatilia kwa kalibu kikao hicho katikati Mkuu wawilaya ya Mlele Majidi Mwanga |
Amesema maboresho ya kodi yakifanyika kwa wafanyaniashara wa Katavi kutasaidia kulipa kodi na kuleta maendeleo kwenye Mkoa na nchi kwa jumla kutokana na furusa nyingi za uwekezaji zilizopo katika Mkoa wa Katavi .
Mwenyekiti wa Jumuia yaWafanya biashara Tawi la
Mkoa wa Katavi Amani Mahella amesema ni ukweli usiopingika kuwa kumekuwepo na utitiri wa tozo kwa wafanya
biashara hali ambayo imekuwa ikipelekea watu ambao wanataka
kufungua biashara kukata tamaa na
kushindwa kufungua biashara .
Ameeleza kuwa kodi ya thamani imekuwa ni changamoto kubwa kwa baadhi ya wafanya biashara kama wa hotel ambao wateja wao wanakonunua bidhaa kama kuku ,viongo na matunda ni wafanya biashara wanao uza bila kuwapatia risiti
Anna Nchagwa mwakilishi wawatu wenyeulemavu akiwasisilisha ombi kwa serikali kupunguza kodi ya vifaa vya watu wenye ulemavu ili viweze kuuzwa kwa bei rafiki. |
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanya biashara Wilaya ya Mlele Sebastian Haule amesema mashine za EFD zimekuwa sio rafiki kwa wafanya biashara hivyo ameiomba Serikali kupitia kwa wataalamu wake kukaa na kufikiria upya njia ya kutengeneza mashine zitakazokuwa zinahesabu pesa itaweza kusaidia kuwabana wafanya biashara wanao kuwa wanatoa taarifa zao ili kukwepa kodi .
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga
alishauri kuwepo na utoaji wa
leseni kwa viwango tofauti kwa wale
wanatumia vyombo vya moto kuendesha kwa
starehe leseni zao za udereva
ziwe juu itasaidia kuongeza mapato
zaidi ya Serikali.