Meneja wa Tanroads Mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende [Katikati] akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa Daraja la Mirumba kwa Naibu waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfley Kasekenya [kulia] |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Wakala wa Barabara TANROADS Mkoa wa Katavi wameanza kutekeleza miradi mitatu mikubwa ya madaraja yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 17.2 itakayo ondoa changamoto kwenye madaraja hayo kwa watumiaji wa Magari na wasafiri .
Naibu waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfley Kasekenya akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mirumba litakalogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 6 .3
Wakala wa Barabara TANROADS Mkoa wa Katavi wameanza kutekeleza miradi mitatu mikubwa ya madaraja yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 17.2 itakayo ondoa changamoto kwenye madaraja hayo kwa watumiaji wa Magari na wasafiri .
Memeja wa Tanroads Mkoa wa Katavi Mwandisi Martin Mwakabende ameyasema hayo wakati alipokuwa akitowa taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Mwandisi Godfery Kesekenya wakati alipokuwa akikagua mradi wa daraja la Mirumba linalounganisha Mikoa ya Katavi na Rukwa
Mwakabende amesema Tanroads mkoa wa Katavi wamefanikiwa kupata miradi mitatu mikubwa ya ujenzi wa madaraja yanayojengwa na Serikali kwa ufadhili wa fedha za Benki ya Dunia yenye thamani ya gharama ya TSH 17,286,798,663.5 .
Ameitaja miradi hiyo mitatu kuwa ni daraja la mto Katuma(Sitalike) linalounganisha mikoa ya Katavi na Rukwa lenye urefu wa km 0+ 420 ambalo ni utatuzi wa changamoto ya muda mrefu kwenye usafiri litakalo gharimu zaidi ya shilingi Bilioni 9.1
Mengine ni madaraja ya mirumba lenye urefu wa mita 60 na upana wa mita 20 lenya thamani ya tshs 6,399,538.440.00 daraja ambalo litaruhusu magari kupita bila kizuizi chochote cha uzito tofauti na la sasa la chuma linaruhusu magari yenye uzito wa tani 38 tuu mradi mwingine ni wa nadaraja Box culverts 16 kwenye barabara ya Maji Moto kwenda Kilida utakao gharimu Tsh 1.781,051,262.50.
Mwakabende amefafanua kuwa miradi hiyo yote mitatu itefanywa na wakandarasi watatu wa Kitanzania na itasimamiwa na Wahandisi washauri kutoka ofisi ya Tanroads Mkoa wa Katavi na itatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja .
Naibu Waziri Mwandisi Godfery Kasenya amesema Serikali inagemea kuona kuona ujenzi wa miradi hiyo inatekelezwa kwa ubora na kwa kiwango kikub wa na kumalizika kwa wakati kwani fedha za miradi hiyo zote zipo tayari .
Amesema miradi hiyo yote mitatu inatekelezwa na wakandarasi watatu hivyo ni kipimo kwa wakandarasi hao hivyo wanatakiwa waonyeshe kuwa wanauwezo wa kufanya miradi mikubwa kwa ubora na kwa muda .
Muonekano wa Daraja la Mirumba linalotumika kwa sasa na wananchi wa Kijiji cha Mirumba
Amebainisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anataka wakandarasi wazawa wakuwe na fedha wanazozipata zinabaki hapa nchini kwa hari hiyo wakandarasi wazawa wano hukujumu la kumwakikishia Rais kuwa wao uwezo wa kutekeleza miradi mikubwa .
Mkazi wa Kijiji cha Mirumba Halmashauri ya Mpimbwe Paulo Katavi amemshukuru Rais Dkt Samia kwa kupeleka mradi huo wa daraja kubwa la Mirumba .
Amesema wamekuwa wakiteseka sana kutokana na daraja la mto huo kuwa linakatika mara kwa mara kutokana na magari yenye uzito mkubwa yaliyokuwa yakipita kwa ajiri ya kusafirisha mazao kupeleka kwenye Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Mkoa wa Rukwa .