Na Mwandishi wetu, Mjombe.
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited ambaye atahudumia wilaya zilizopo ndani ya Mkoa wa Njombe kwa kuuza kwa bei ya ruzuku mitungi ya gesi ya kilo sita pamoja na vifaa vyake katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji.
Hayo yamebainishwa leo Januari 4, 2025 mkoani Njombe na Mhandisi wa
miradi wa REA, David Malima wakati wa
uzinduzi rasmi wa mradi wa ugawaji mitungi ya gesi ya kilo sita Kata ya
Tandala, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.
Mha. Malima amesema kuwa mitungi ya gesi 13,020 itakayosambazwa mkoani
Njombe itachochea kwa kiasi kikubwa matumizi ya nishati safi na salama.
"Lengo la mradi ni kukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresha
upatikanaji wa huduma za nishati safi ya kupikia ili kupunguza ukataji wa miti
ambapo takribani hekta 400,000 hukatwa kila mwaka, " Amesisitiza Mha.
Malima.
Amezitaja wilaya zitakazonufaika kuwa ni pamoja na Wilaya ya Makete, Ludewa,
Njombe na Wanging'ombe.
Kwa upande wake, Mtendaji wa kata ya Tandala , Bw. Maximillian Msigwa
ameipongeza REA kwa kuja na mradi huo na kuiomba iwe endelevu ili iweze
kuwasambazia wananchi wengi nishati hiyo muhimu Na kuchochea ustawi wa maisha
ya wananchi.