![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizumgumnza na watendaji mbalimbali wa Mkoa wa Katavi wakati wa uzinduzi wa Mpango mkakati wa kukabiliana na udumavu. |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Mkoa wa Katavi
umeanza kufanya jitihada ya kuhakikisha tatizo la
lishe duni linatokomezwa huo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais alilolitoa kwa viongozi wa Mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake aliyoifanya katika Mkoa huo Julai Mwaka jana
.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko[kulia]akimkabidhi mpango mkakati wa kukabilina na udumavu Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Albert Msovela |
Mkoa wa Katavi umeanza kufanya jitihada ya kuhakikisha tatizo la lishe duni linatokomezwa huo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais alilolitoa kwa viongozi wa Mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake aliyoifanya katika Mkoa huo Julai Mwaka jana .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema kuwa katika kuhakikisha wanatekeleza
agizo la Rais Mkoa huo umezindua
rasmi kazi ya mkakati wa
kutokemeza tatizo la udumavu
nakuimarisha hali ya lishe kwa
wananchi wa Mkoa wa Katavi
Uzinduzi wa mkakati huo umezinduliwa
na Mkuu wa Mkoa wa Katavi katika ukumbi
wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na uliudhuliwa na viongozi wa kutoka Halmashauri zote tano za Mkoa wa huu,viongozi wa madhebu ya dini, vyama vya
siasa , viongozi wa kimila ,wazee
maarufu na wadau mbambali waliko
katika mkoa wa Katavi .
Mrindoko
amesema lengo walilonalo ni kuondoa kabisa tatizo hilo kama ambavyo walivyoagizwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake aliyoifanya hapo mwaka
jana katika Mkoa wa Katavi hapo Julai 24 mwaka jana .
Amesema wameanza safari kwa kuzindua mpango mkakati wa utekelezaji wa kazi ya kutokemeza
udumavu na lishe mbaya ambapo hivi karibuni walikwenda Mkoani Njombe kujifunza
jinsi mkoa huo unavyo fanya juu ya
kupunguza tatizo la udumavu na lishe mbaya .
Amesema wamezindua kamati maalumu
ambayo itakuwa inafanya kazi kila siku
mpaka ambapo watakapokuwa wamehakikisha udumavu umetokomezwa kabisa katika Mkoa huu kwa maana hiyo kila mmoja na kwa kila
mdau watambue kuwa wanayokazi ya
kufanya ya kutoa ushirikiano wa kumaliza tatizo hilo .
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi
Albert Msovela alisema wakati wa ziara ya Rais mwaka jana aliwaagiza
waende wakajifunze kwa wenzao wa Njombe
jinsi walivyoweza kufanya
mikakati ya kupambana na hali ya
udumavu na timu hiyo iliongonzwa na Mkuu
wa Mkoa wa Katavi.
Alieleza kuwa kutokana na ziara hiyo wameweza kujifunza namna ya kupambana kutokomeza tatizo hilo na ndio maana kama
mkoa wameanza utekelezaji kwa kuzindua mkakati wa kutokomeza tatizo hilo
kwa wananchi .
Na Mzee
Maarufu Vicenti Nkana amesema
kuwa tatizo la udumavu
kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi limekuwa likichangiwa na tabia ya
wananchi kupenda kula mlo wa chakula cha
aina moja .
Ameshauli Halmashauri za mkoa huu
kuanzisha sheria ndogo ambayo
itamtaka kila mtu mwenye nyumba kupanda miti ya matunda mitano .