Kapufi; Kuongezeka kwa idadi ya watu sio balaa.

 

Mwenyekiti wa TPAPD na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi akitoa mada katika mkutano wa athari ya ongezeko la watu dunuani.

Mwenyekiti wa TPAPD na Mbunge wa Jimbo la Mpanda mjini Sebastian Kapufi, ameeleza kuwa upatikanaji wa vifaa vya kisasa na huduma bora katika sekta ya afya umechangia kupunguza idadi ya Watanzania kwenda kupata matibabu nchini India.

Kupungua kwa idadi kubwa ya watu kutafuta matibabu nchini India umetajwa kuchangiwa na kazi nzuri inayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye uboreshaji wa miundombinu ya sekta ya afya.

Kapufi akizungumza Februay 25, 2025  katika Mkutano wa Wabunge wa Afrika na Asia juu ya idadi ya watu na maendeleo ukijadili jukumu la wabunge katika kuunganisha takwimu za idadi ya watu ili kukuza ujumuishaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, amesema maendeleo yoyote yanategemea afya ya watu.

Mwenyekiti huyo wa TPAPD akiwa jijini Dar es salaam, aliweka wazi kuwa uboreshwaji wa huduma za afya hosptali ya Muhimbili na uimarishwaji wa huduma hosptali ya Amana na Mwananyamara umeondoa kero ya watu kutafuta matatibabu nje ya nchi.

Alisema ukiwa na jamii ambayo haina afya bora mambo yote yanayopangwa kufanywa yanakosa maana jambo ambalo serikali imefanya kazi nzuri na kubwa ya kuimarisha eneo hilo la afya  kwa kujenga kila pembe ya nchi zahanati, vituo vya afya na hosptali.

Akizungumzia athari la ongezeko la watu ulimwenguni, Kapufi amefafanua kuwa TPAPD imeona mtoto wa kike kwa namna gani anaweza kunusuliwa na mambo mbalimbali ili aweze kushiriki kwenye uchumi wa nchi huku wakiangalia idadi ya watu kuweza kuwa neema na sio balaa.

“Ni mambo gani ambayo yanaweza kufanya idadi ya watu ikawa balaa…Kwa mfano kuwa na idadi kubwa ya watu sio tatizo lakini idadi kubwa ya watu ambao huwezi kuwahudumia ndio tatizo linaanzia hapo” alisema.

Alifafanua idadi kubwa ya watu hapa nchini imeweza kuhudumiwa kwa serikali kuimarisha miundombunu mbalimbali  katika sekta ya afya na ujenzi wa miradi mingine mikubwa.

Sipika wa Bunge la Jamuhuri wa Muugano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson akiwa mgeni rasmi katika mkutano huo.

Waziri wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Afrika Kusini Pemmy Majodina, amesema kuwa Bara la Afrika limeathiliwa na mimba za utotoni nani vigumu kudhibiti kama idara ya afya na hosptali bali inategemea wazazi na jamii kuona ni nini cha kufanya kujenga jamii  sio ya kutibu dalili bali kuwa na jukumu la kuzuia kama wazazi na wategeneza sheria na sera.

Majodina alieleza kuwa kuna umuhimu wa kuwekeza zaidi katika taasisi za afya kwani uwekezaji kwa watu maana yake ni kuwekeza kwenye afya.

“Leo hapa tunadhibitisha kwamba tunachukua jukumu la afya mikononi mwetu kwa sababu uzaishaji wa taifa unategemea taifa la Tanzania lenye afya” alisema.

Aidha amewapongeza serikali ya Japan kwa kufanya kazi nzuri ambayo sio ya kuwadhoofisha kwa kufanya kila jambo kwa usawa.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages