WANANCHI WAILALAMIKIA TARURA KWAKUHATARISHA USALAMA WAO.

 



  Moja ya Nyumba inayo lalamikiwa na mkazi wa mtaa wa Sokoine kata ya Kashaulili ambayo mmiliki wa nyumba hiyo amekuwa akiingia kwa tabu kwenye nyumba yake kutokana na vifusi vya udongo vilivyokuwa kwenye mtaro na kusambazwa kwenye eneo lake na mkandarasi wa (TARURA).


Mpanda-Katavi.

Na  Mwandishi wetu

Wananchi katika Halimashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameilalamikia mamlaka ya barabara za mjini na vijijini (TARURA) kuzibua mitaro na kuhamishia udongo kwenye nyumba zao.

Wakipaza sauti kwa vyombo vya habari wananchi wa mtaa wa Sokoine Kata ya Kashaulili Manispaa ya Mpanda Katavi wamesema changamoto hiyo uwenda  ikapelekea maafa makubwa  kama kubomokewa nyumba zao kutokana na mvua zinazo nyesha .

Idd Mvano Mkazi wa mtaa  Sokoine kata ya Kashaulili ametaja kukumbana na changamoto ya njia wakati wa kuingia na kutoka nyumbani kwake kutokana na njia kuzibwa na udongo unao tolewa kwenye mitalo na kuwekwa pembeni mwa nyumba.

Katika hatua nyingine Zuber Maulidi ambae pia ni mkazi wa wa maeneo hayo ameioba (TARURA) kuchukua hatua za haraka kuondoa udongo uliopo katika nyumba zao na kutoa elimu kwa wakandarasi wanao zibua mitaro ili wananchi waweze kuepuka changamoto hizo.

Nao baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Ikulu kawajense wanawaomba  TARURA  kuona namna ya  kufanyia usafi baadhi ya barabara zilizopo kati  kati ya  Mji wa Manispaa ya Mpanda  kwa   kufyeka nyasi zilizopo pembezoni mwa barabara  hali  ambayo imekuwa ikihatarisha  usalama wa watembea kwa miguu na watumiaji wa vyombo vya moto .

Moja ya barabara iliopo katika Manispaa ya Mpanda eneo la Waiti Jirafu ambayo watembea kwa miguu na watumiaji wa vyombo vya moto wako hatarini kupoteza maisha kutokana na barabara hiyo kuwa na nyasi ndefu zilizo enea pembeni mwa barabara.
    

Geoge Maiko amaitaja barabara mojawapo ambayo nihatarishi inayo toka baa maarufu ya Waiti Jirafu kuelekea Laiki vyu nimiongoni mwa barabara ambayo ni hatarishi sana kwa watembea kwa miguu na watumiaji wa vyombo vya moto kutokana na barabara hiyo kuwa na nyasi nyingi pembeni mwa barabara hali inayopelekea sehemu inayo tumiwa abayo haina nyasi kuwa ni ndogo hata magari yamekuwa yakipishana kwa shida.

 Muonekano wa barabara kwa watembea kwa miguu na watumiaji wa vyombo vya moto na watembea kwa miguu iliopo katikati ya mji wa Mpanda.

 

 


 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages