Na Walter
Mguluchuma, Katavi.
Wananchi wa
Mkoa wa Katavi wa jinsia zote wamealikwa
kushiriki maadhimisho muhimu ya
siku ya Wanawake Duniani ambayo
yatawashirikisha wanawake wote wa mkoa huo
ili kusherekea kwa pamoja na kujiwekea
mikakati itakayo wawezesha wanawake kufikia malengo yao ya
ustawi wa kiuchumi.
Wito huu
umetolewa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa
ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya
wanawake Duniani ambapo kimkao yatafanyika
katika uwanja wa Kashaulili
Manispaa ya Mpanda.
Alisema maadhimisho hayo muhimu yatawashirikisha wanawake wote na wananchi wa Mkoa huu ili kuweza kusherekea kwa pamoja na kujiwekea mikakati mbalimbali ili kuweza kufikia malengo ya ustawi wao wa kiuchumi.
Hivyo wananchi wote, Wadau wa maendeleo , Taasisi
za umma na binafsi, Viongozi wa dini na vyama vya siasa wanaalikwa kwenye maadhimisho hayo.
Buswelu
alisema kwenye maadhimisho hayo yataambana na shughuli mbalimbali ambapo baadhi ya shughughuli hizo ni kufanya
kongamano la wanawake , kuwatembelea watoto walio kwenye mazingira magumu na kuwafanyia matendo ya huruma na kutembelea
mradi wa machinga.
Amefafanua
kuwa mwaka 1977 Umoja wa Mataifa ulipisha azimio lililozitaka
nchi wanachama kila ifaikapo
machi 8 kila mwaka kufanya maadhimisho haya ili kuenzi
mchango wa mwanamke
katika ujenzi wa Taifa husika
kwa Tanzania siku ya mwanamke Duniani
ilianza kuadhimishwa 1997.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni wanawake na wasichana 2025 tuimarishe haki usawa na uwezeshaji.