MTANDAO WA POLISI WANAWAKE KATAVI WATEMBELEA GEREZA MPANDA NA KUTOA MSAADA

Na Daniel kimario-Katavi

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Dunia yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa Machi 8, mwaka huu Mkoani Arusha Mtandao wa Polisi wanawake (TPF - NET) Mkoa wa Katavi  Machi 4, 2025 wametoa mahitaji ya vitu mbalimbali kwa mahabusu na wafungwa wa Gereza la Mahabusu Mpanda. 

Msaada huo umetolewa kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani na Mrakibu wa Polisi (SP) Sanjukila Wagesa akiambata na wakaguzi pamoja na askari wa vyeo mbalimbali.

Mahitaji yaliyotolewa ni pamoja na juice, biscuti, kanda mbili, taulo za kike, mchele, mafuta ya kupaka, pampasi za watoto, nguo za ndani, sabuni ya unga na kipande, dawa za meno, miswaki na maziwa ya watoto.

 Akipokea msaada huo Kaimu Mkuu wa Gereza la Mahabusu Mpanda Mrakibu Msaidizi wa Magereza James Sapi amewashukuru Jeshi la Polisi wanawake mkoa wa Katavi na kusema msaada huo utakwenda kuwafanya wahitaji hao kujiona bado ni sehemu ya jamii

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages