![]() |
Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika (LATCU) Mkoa wa Katavi Pius Kilo. |
Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Katavi(LATCU )kimeanza kufanya kazi zake kwa kutumia mfumo wa Tehama na wamejipanga kuhakikisha vyama vyote vya Msingi wanavyovisimamia navyo viaze
kufanya kazi kwa kutumia mfumo wa TEHAMA.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni
na Meneja Mkuu wa Chama kikuu cha ushirika (LATCU)cha Mkoa wa Katavi Pius Kilo, wakati wa nkutano mkuu wa 31 wa
chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa
ya Mpanda
Amesema Dunia ipo katika sura za taasisi zote ziwe katika mfumo wa Kidigitali yaani kwamba shughuli zote ziwe ni za Kitehama na wao kama LATCU hawakubaki nyuma yatari wanao mfumo wa Tehama unao fanya kazi
Hivyo wao kama LATCU wanao jukumu kubwa la kuhakikisha vyama vyao vya msingi vyote wanavyovisinania katika Mkoa wa Katavi na vyenyewe pia vinakuwa na mfumo wa Tehama .
Amewasisitiza vuongozi wa Amcos
na watendaji kufanya kazi kwa uaminifu
na uadilifu mkubwa na sio kuishia
hapo pamoja na wakulima
wenyewe wanapaswa kuwa hivyo
ili kuweza kufanya
madeni yote yanayokopwa kwenye mabenki yaweze kulipika yote .
Kilo ameeleza kuwa
kama wakulima wasipokuwa
waadilifu na waaminifu kunaweza
kusababisha kushindwa kurejesha
madeni ya pembejeo yanayokuwa
wamekopeshwa na Mabenki kupitia
Amcos zao na wanapo shindwa kukopesheka
wakulima wanashindwa kuendelea.
Nae Richald Zengo Mrajisi Msaidizi anae simamia vyama visivyo vya kifedha kutoka tume ya maendeleo ya vyama vya ushirika wao kama wasimamizi wao jukumu la kuhakikisha vyama vyote vya ushirika vina kwenda vizuri.
Amesema bado kuna baadhi ya vyama viongozi wake wamekuwa sio waadilifu hivyo anapenda kuwakumbusha kuwa hawatasita kuwachukulia hatua viongozi ambao watakuwa hawana uadilifu .
Amesisitiza kuwa sasa hivi
wakulima wanaendea kwenye
msimu wa masoko na moja ya
uadilifu ni baadhi ya wakulima wa tumbaku wamekuwa wakitorosha tumbaku yao na wengine wamekuwa hata madeni hawalipi
hivyo vuongozi wahakikishe wale
wote waliokopeshwa na mabenki wanalipa
ili Amcos ziendelea kuwa na fisa za
kukopesheka .
Ameikumbusha LATCU
kuhakikisha changamoto zimazokuwa
zinatokea kwenye Amcos wasishughulikie mapema
wasibiri mpaka mrajisi msaidizi wa Mkoa ndio ashughulikie .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Nsimbo Amcos Credo Kasokola ni kweli kwenye baadhi ya Amcos wamekuwa sio waaminifu na wamekuwa wakisababisha kuwepo kwa madeni wengine ni kwa makusudi na wengune kwa kutofahamu.