![]() |
Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Katavi Mhadisi Albart Laizer. |
Na Walter Mguluchuma, Katavi.
Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Katavi
wamepata mwarobaini wa kuondoa changamoto iliyokuwepo kwa
muda mrefu wakati wa kipindi cha
mvua kwenye daraja
la Sitalike linalounganisha Mkoa
wa Rukwa na mikoa mingine ya nyanda za juu kusini.
Kaimu Meneja wa
TANROADS Mkoa wa Katavi Mhandisi
Albart Laizer hivi karibu
amesema Wizara ya Ujenzi imetowa
kiasi cha shilingi Bilioni 9.3 kwa ajili ya ujenzi wa
daraja la Sitalike lenye
urefu wa mitaa 55 linalouganisha
Mkoa wa Katavi na Mkoa wa Rukwa ambalo lilikuwa na changamoto kwa muda
mrefu wakati wa kipindi cha masika.
Amebainisha kuwa ujenzi wa baraja hilo umeisha anza na unatekelezwa na kampuni ya kizawa ya Mselemu ya Mkoani Rukwa kwa fedha za Benki ya Dunia ambapo ikumbukwe kuwa baada ya mvua za mwaka jana daraja linalotumika kwa sasa lilisimama kwa kipindi cha mwezi mmoja na hali ambayo iliwalazimu watumiaji wa barabara inayopita katikati ya Hifadhi ya Katavi watumie barabara ya Kibaoni-Sitalike.
![]() |
Ujenzi wa Daraja la Sitalike ambalo linauganisha Mkoa wa Katavi na Rukwa ambalo litakuwa msaada mkubwa wa kuuganisha mawasiliano ya mikoa hiyo miwili. |
Ameeleza kuwa faida
kubwa ya mradi huo wa daraja utaondoa
kabisa changamoto iliyokuwa inaendelea
hasa nyakati za masika kwa maana daraja
lililopo kwa sasa ni dogo na kufanya lifelike
wakati wa kipindi cha masika hasa
kwenye kipindi cha miezi ya Januari hadi
Aprili sasa baada ya kukamilika kwa
daraja hili litakuwa linapitika kipindi chote
itakuwa ni sululisho la kudumu.
Mbali ya Daraja hili wanajenga pia
madaraja mengine ambayo ni
daraja la Milumba lenye urefu wa mita 60 linalogharimu kiasi cha fedha kiasi cha
shilingi Bilioni 6.3 muda wa utekelezaji
ukiwa ni miezi 15.
Daraja la tatu ni la Kilida ambalo wakati wa mvua lilikuwa lilikata mawasiliano kati ya wananchi wa bonde la Rukwa na Mpimbwe ambapo ujenzi wake utaghalimu shilingi Bilioni 1.78 nalo linajengwa kwa fedha za Benki ya Dunia.
![]() |
Hili ni daraja la Sitalike ambalo hapo awali lilikuwa linatumiwa na wananchi wa mikoa miwili ya Katavi na Rukwa. |
Mkazi wa kata ya Sitalike wilaya ya Mpanda, Salum Sanga amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea ujenzi wa daraja ambalo ni daraja muhimu linalounganisha mikoa miwili ya Katavi na Rukwa kwani kutaondoa ajali nyingi ambazo zilikuwa zinatokea.
Bahati Bitus amesema kwa kumbuku kumbu zake kuna ajali tatu
ziliwahi kutokea siku za nyuma ikiwemo iliyohusisha bus moja la Kampuni ys
Sumry lilopata ajali na watu zaidi ya kumi walipoteza maisha.
Aidha ameshukuru hatua nzuri zilizochukuliwa na serikali ya
kuanza ujenzi wa daraja hilo jipya
linalojegwa kwani wanaimani litakuwa mkombozi kwao kwa kupunguza au kumaliza
kabisa tatizo la ajali katika eneo hilo.