![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwamamvua Mrimdoko [Kulia] akimkabidhi ufunguo wa Pikiki Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi Walter Mguluchuma. |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Mwanamvua Mrindoko amekabidhi Pikipiki moja kwa klabu ya waandishi wa Habari
Mkoa wa Katavi kwa lengo la kusaidia kuifikia jamii kwa urahisi katika
utekelezaji wa majukumu ya kihabari.
Walter Mguluchuma Mweyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari[kushoto]akitoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko baada ya kukabidhi Pikipiki hiyo kwa waandishi wa Habari. |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amekabidhi Pikipiki moja kwa klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi kwa lengo la kusaidia kuifikia jamii kwa urahisi katika utekelezaji wa majukumu ya kihabari.
Akikabidhi Pikipiki hiyo kwa viongozi wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi,Mkuu huyo wa mkoa amesema lengo la kutoa chombo hicho cha usafiri ni kuwafikia wanananchi wa maeneo mbali katika majukumu ya kihabari na katika kutatua changamoto zao pamoja na kuziona kazi mbalimbali zinazofanywa na serikali kwa wananchi.
‘’Nakukabidhi rasmi pikipiki hii ili kurahisisha kazi za kihabari na kuwafikia wananchi maeneo ambayo wananchi ambao hawawezi kuwafikia waandishi wa habari kwa uharaka’’Mrindoko.
Ameeleza kuwa kupitia
pikipiki hiyo itasaidia kupata mrejesho wa kazi zinazofanywa na serikali ya
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia habari pindi watakapo fikiwa na waandishi
wa habari katika maeneo yao.
Mrindoko amewaomba waandishi wa habari kuendelea kuonyesha ushirikiano na serikali na wadau mbalimbali kama ambavyo wamekuwa wakionyesha kupitia kazi mbalimbali za kihabari kwa wananachi na jamii nzima kwa ujumla.
‘’Niwaombe kuzingatia
sheria kanuni na maadili katika utendaji wenu wa kazi kwa mkoa wetu wa katavi
sina wasiwasi mnafanya kazi zenu vizuri tunawashukuru kwa namna mnavyo utangaza
mkoa wetu wa Katavi’’Mrindoko.
Walter Mguluchuma Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Katavi amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua mrindoko kwa kuona umuhimu wa kuwapatia usafiri huo waandishi wa habari kwakuwa utasaidia kuwafikia wananchi kwa usalama na kwaharaka zaidi.
Mguluchuma amesema kuwa
waandishi wa Mkoa wa Katavi wataendelea kufanya kazi na serikali ya mkoa wa
Katavi na serikali kwa ujumla.
Amesema kuwa uongozi wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania [UTPC] kupitia kwa Mkurugenzi wa UTPC Taifa Keneth Simbaya amemshuru Mkuu wa Mkoa wa Katavi kwa kuonesha mfano hai kwa kutambua mchango wa waandishi wa habari wa Mkoa wa Katavi.