MKOA WA KATAVI WAPITISHA MAPENDEKEZO Y A BAJETI ZAIDI YA BILIONI 164

 

Kaimu  Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi  Makongoro  Nyerere akiongoza kikao cha Kamati ya ushauri Mkoa wa Katavi


Na Walter Mguluchuma-Katavi

Kamati ya  ushauri ya  Mkoa wa Katavi (RCC) imepitisha mapendekezo ya  rasmu ya  Bajeti  ya  ofisi ya Mkuu wa Mkoa na  Halmashauri zake  tano  ya zaidi ya   shilingi Bilioni 164 ikiwa imezingatia kuwaletea wananchi  maendeleo  na kutatua kero mbalimbali  za wananchi .

Kamati ya  ushauri ya  Mkoa wa Katavi (RCC) imepitisha mapendekezo ya  rasmu ya  Bajeti  ya  ofisi ya Mkuu wa Mkoa na  Halmashauri zake  tano  ya zaidi ya   shilingi Bilioni 164 ikiwa imezingatia kuwaletea wananchi  maendeleo  na kutatua kero mbalimbali  za wananchi .

Mapendekezo hayo  ya rasmu ya  bajeti  yamepitishwa  katika  kikao  cha  Kamati ya  ushauri ya  Mkoa  wa Katavi  kilichofanyika  katika  ikumbi wa ofisi  ya  Mkuu wa  huu  kilichoongozwa na  Kaimu  Mkuu wa  Katavi  Makongoro  Nyerere ambae pia ni  Mkuu wa  Mkoa wa Rukwa .

Akiwalisha  mapendekezo   ya bajeti hiyo mbele ya wajunbe wa kikao Mtakwimu wa  Mkoa wa Katavi    Grace  Madaha  amesema  Ofisi ya  Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi pamoja na  Halmashauri zake zote tano za  mkoa huu  wameomba  kupitishiwa  kwa  mwaka wa fedha wa 2025/ 2026 kiasi cha  shilingi Bilioni  164, 928,709,000 .

Madaha  ameeleza kuwa     kwa  mwaka wa  fedha wa 2024/ 2025  Mkoa  huu  ulipitisha shiwa kiasi  cha  fedha  shilingi Bilioni  153. 3 kwa ajiri ya  ofisi  ofisi ya   mkuu wa Mkoa na  Halmashauri zake  kwa ajiri ya kutekekeza  mahukumu yake .

Amesema  mapendekezohayo ya bajeti yamezingatia vipaumbele  mbalimbali ambavyo amevitaja kuwa ni  kuinarisha  na kuboresha maeneo ya utawala  afya ,elimu  na  umaliziahi wa miradi vipolo pamoja  na umaliziaji wa maboma 500 ya shule ambapo kila  Halmashauri ya Mkoa huu inaidadi ya maboma  100.

Ametaja vipaumbele  vingine kuwa ni  usimanizi wa mazingira ,mabadiliko  ya  tabia ya  nchi  kwa  kuandaa  mpango wa  kuhifadhi  mazingira , kuwezesha  wananchi kiuchumi  kupitia  utowaji wa mikopo  ya asilimia kumi  kwa kupitia  mwongozo   mpya   wa   mwaka 2024 kwa  vikundi vya wajasiriamali  wanawake   vijana  na watu  wenye  ulemavu.

Kupeleka  miradi ya  Maendeleo kwa kufuata  madaraja  ya asilimia 20   asilimia 40 na asilimia 60 na  kutenga  bajati kwa  ajiri ya kupima  maeneo ya   taasisi   zilizoko katika  Halmashauri   pamoja na shule   vituo vya kutolea   huduma ya  afya na kuimarisha  utawala  bora  na demokrsia,

 Madaha  amesema Pia wamepanga     kutenga  fedha kwa ajiri ya kuilipa  madeni ya watumishi   wazabuni na wakandarasi  na kujenga  majengo ya  utawala ya  Halmashauri  na nyumba za  baadhi ya watumishi  ofisi ya  mkuu wa   Mkoa na  Halmashauri

Mwenyekiti wa  Halmashauri ya  Mpimbwe  Sailas  Ilumba  aliwasilisha  ombi  la kuomba  kutatuliwa  kwa  migogoro ya mikapa  kati ya wananchi  wa  Halmashauri ya   Mpimbwe na  wananchi wa  Halmashauri ya Sumbawanga  Vijijini ,

Kwa  upande wake  Kaimu  Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi  Makongoro  Nyerere amewaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa  kuwa swala   hilo  la migogoro ya utawala   lisiwafanye  wanaishi wanao ishi  kwenye maeneo  hayo  yenye  migogoro ya kimipaka yasiwafanya wananchi washindwe  kufanya kazi zao za  maendeleo .

Hivyo  amewataka  viongozi  wa   mikoa  hiyo  miwili  wasikubali  kukaa na  migogoro  kama  hiyo  ambayo inazungumzika  hivyo  ameshauri kifanyike kikao cha pamoja  kuhadili  swala hilo na kulitatua kwa  haraka sana .

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages