![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko |
Na Walter Mguluchuma
Katavi.
Mkoa wa Katavi wamezindua mpango mkakati wa kuondoa tatizo la udumamavu unao tokana na lishe duni ikiwa ni itekelezaji wa agiza la Rais alilolitokoa mwaka 2024 kufatia mkoa huo kuwa na idadi kubwa ya watu wemye udumavu .
Uzinduzi huo wa mpango wa kuondoa tatizo laudumavu na lishe duni umezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda na kuhudhuriliwa na viongozi wa Mkoa na Wilaya zote za Mkoa wa wananchi ,viongozi wa dini, kimila pamoja na wananchi mbalinbali na wahasiliamali .
Rc Mrindoko amesema kuwa sote tunatambua kuwa hali ya udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano katika Mkoa wa Katavi bado ni changamoto kubwa kwa mujibu wa takwimu kuwango cha udumavu katika Mkoa huu ni asilimia 32.2 sawa na watoti 60,730 hali ambayo hairidhishi kwani ipo juu ya wastani wa kitaifa ambayo ni asilimia 30.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko akikagua baadhi ya mabanda wakati wa uzinduzi wa kampeni endelevu ya kupunguza udumavu unaosababishwa na lishe duni |
Katika kukabiliana na changamoto hiyo ndio maana Mkoa huo umeweka mikakati mbalilimbali kwa kuweza kufanya uzinduzi wa Kampeni ya Mkoa ya kupambana na udumavu kwa dhati kabisa kwenye maeneo yote ya Mkoa huu .
Amebanisha kuwa katika ziara yake aliyoifanya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mwaka hana kwenye Mkoa huu aliwaagiza viongozi wa Mkoa waende mkoa Njombe wakajifunze njia bora ya kutokomeza tatizo la udumavu unaotokana na ukosefu wa lishe bora na tayari wameisha tekeleza agizo hilo kwa kwenda kujifunza Njombe .
Amesema wananchi wa mkoa huu wanapaswa watambue kuwa bado wanayo kazi kubwa ya kufanya kwani tatizo hilo lipo kwenye mkoa hivyo wanao wajibu wakushirikiana kwa kuhakisha jambo hii la mkakati wa kutokomeza tatizo hilo lina mgusa kila mwanamchi wa Mkoa wa Katavi
Amefafanua kuwa walipo kuwa Mkoani Njombe waliweza kujifunza pia nanma ya utoaji wa lishe bora kwenye shule na tayari na tayari wamefanya hivyo kwenye baadhi ya shule iliwepo shule ya sekondari ya Simbwesa kwa kuweza kuwapatia Ng/ombe kwa ajiri ya maziwa .
Amewasisitiza wananchi kuzingatia ulaji wa lishe bora kwa kuzingatia milo ya aina sita na pia wananchi wapende kula matunda ya asili yanayopatikana kwenye Mkoa wa Katavi kwani yanaweza kuwa na vilutubisho kuliko matunda ya sehemu myingine .
![]() |
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Albert Msovela akitoa ripoti ya mpango wa haraka kupunguza udumavu |
![]() |
Baadhi ya maofisa ya serikali ya mkoa wa Katavi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupunguza udumavi |
Amesema mkoa huiu haina sababu yoyote ya kufanya washindwe kumaliza tatizo hilo kabisa kwa njinsi ambavyo mikakati ilivyoandaliwa vizuri na uongozi wa mkoa huu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Albart Msovela amesema hadi sasa juhudi balimbali zimeisha anza kufanyika na kutekelezwa ili kukabiliana na changamoto hiyo ikiwa na pamoja na kuundwakwa kamati mbalimbali ngazi ya Mkoa ,Halmashairi mpaka ngazi za vijiji mitaa na vitongoji
Kaili mbiu ya mkakati huo wa Mkoa wa Katavi ni LISHE BORA AFYA YAKO ZIMGATIA UNACHO KULA