Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi,Walter Mguluchuma Kushoto akitoa shukrani za UTPC kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi. |
Na Mwandishi wetu Katavi
Muungano wa Klabu
za Wandishi wa Habari Tanzania(UTPC) wamempongeza Mkuu wa Nkoa wa Katavi Mwanamvua
Mrindoko kwa kuweza
kuwapatia usafiri chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Katavi uatako wasaidia wandishi wa Habari kutekeleza
majukunu yao .
Muungano wa Klabu za Wandishi wa Habari Tanzania(UTPC) wamempongeza Mkuu wa Nkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kwa kuweza kuwapatia usafiri chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Katavi uatako wasaidia wandishi wa Habari kutekeleza majukunu yao .
Pongezi hizo za UTPC zimetolewa na Mwenyekiti wa Klabu ya Wandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi Walter Mguluchuma kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa umoja wa klab za uandishi wa habari Tanzania [UTPC] Keneth Simbaya wakati wa Hafla fupi ya kukabidhiwa pikipiki kwa Klabu ya Wandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko .
Simbaya amesema UTPC inapenda kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kwa msaada wake muhimu wa usafiri wa pikipiki kwa Katavi Press Club ambayo utawahakikishia usafiri pia kuwa kama chanzo cha mapato ya Klabu .
Simbaya ameeleza kuwa ushirikiano kati ya Serikali ya Serikali za Mikoa na vyombo vya Habari ni muhimu kwa mafamikio ya maendeleo ambapo wandishi wa habari wanweza kuwa washirika wa kusaidia kufikisha ujumbe wa Serikali kwa wananchi kutoa maoni ya jamii na kuchangia katika kutatua changanoto za kijamii kwa hivyo msaada wake RC Mrindoko ni mfano wa jinsi Serikali inavyoweza kuimarisha uhusiano na vyombo vya habari kwa manufaa ya wananchi .
Amesisitiza kuwa mfano wake huo wa msaada kwa wandishi wa habari unastahili kuigwa na viongozi wa mikoa mingine hapa Nchini ili vyama vya wandishi wa habari viendelee kitoa hiduma bora kwa wananchi na UTPC wanafurahia sana na roho hii ya ushirikiano na wanaomba kushirikiana kwa pamoja katika kufanikisha malemgo ya maendeleo ya Mkoa wa Katavi na mikoa mingine pia .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko alisema kuwa hana mashaka na utendaji wa kazi na wandishi wa habari kwa namna wanavyo utangaza mkoa kuitia kazi mbalimbai kwenye vyombo vyao vya habari na kama mkoa wataendelea kutowa ushirikiano kwa wandishi wa habari .
Amewataka wandishi wa habari kuzingatia kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao katika kuabalisha umma wa mkoa wa Katavi na Wanzania kwa ujumla wake ameomba wandishi waendelee kufanya kazi kushirikiana na Serikali na wadau wengine wote.
Nae mwandishi wa Habari Paul Mathias amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Katavi kwa msaada huo muhimu ambao utawasaidia kufanyia shughuli za ofisi ya Klab ya Wandishi wa habari pia kuwafikia kwa haraka wananchi wa maeneo ya pembezoni mwa mji pindi kunapokuwa kumetokea matukio mbalimbali .