![]() |
Baadhi ya watoto wakiwa wanaelekea eneo la machimbo Dirifu wakiwa na vitendea kazi. |
Na Mwandishi wetu, Katavi.
Hali ya watoto wadogo
kutumikishwa kwenye shughuli katika maeneo ya uchimbaji madini katika wilaya ya
Mpanda Mkoa wa Katavi limekuwa jambo la kawaida na kupelekea kunyimwa watoto
haki ya kwenda shule.
Wakizungumza baadhi ya watoto wakiwa katika eneo la Dirifu (kutokana na umri wao kuwa mdogo majina yao yameifahidhiwa) wamesema wao limekuwa jambo la kawaida kutokwenda shuleni na badala yake wamekuwa wakifanya shughuli za katika majimbo ya madini na wala hawaulizwi na mtu yeyote.
![]() |
Baadhi ya watoto wakiwa wanaelekea eneo la machimbo Dirifu wakiwa na vitendea kazi. |
“Mimi na rafiki yangu tunaishi
Magamba na hivi mnavyotuona waandishi wa habari ingawa ni muda wa masomo lakini
hatukuweza kwenda shuleni na tuko na vitendea kazi tunakwenda kwenye machimbo
ya madini Dirifu mto Magamba” Amsema mmoja wao.
Ameeleza kuwa wamekuwa wakienda
na kujipatia fedha na mteja wao mkubwa ni Pius ambaye amekuwa akinunua dhahabu
yao wanapokuwa wamepata kwa kiasi cha fedha Tsh 20,000/- hadi Tsh 30,000/-
ambazo zimekuwa zikiwasaidia kwenye mahitaji yao binafsi na familia zao.
Kitendo cha watoto kutumikishwa shughuli za machimboni ni ukiukwaji wa haki za watoto kinyume na sheria za watoto nchini ambapo zinazorotesha ukuaji wao hususani kupitia sekta ya elimu.