Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Taska Mbogo akizungumnza wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya mwaka 2020/2025 |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa KataviTaska Mbogo ametoa zaidi ya shilingi Milioni 249 kwa kipindi cha miaka mitano ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwenye jamii na kwenye Chama cha Mapinduzi kwa Mkoa wa Katavi .
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa KataviTaska Mbogo ametoa zaidi ya shilingi Milioni 249 kwa kipindi cha miaka mitano ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwenye jamii na kwenye Chama cha Mapinduzi kwa Mkoa wa Katavi .
Hayo ameyasema wakati wa
kikao cha Baraza la jumuia ya wanawake CCM(UWT)Mkoa wa Katavi
kilichofanyika katika ukumbi wa idara ya maji uliopo katika Manispaa ya Mpanda
.
Amebainisha kuwa michango
hiyo ameitowa kwa moyo wake na wala kakulazimishwa na mtu yeyote
yule bali ni kutokana na mapenzi aliyonayo ya kuwatumikia wananchi na chama
chake cha CCM.
Amesema hayo ameyafanya kama sehemu yake ya kuwa mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Katavi (ccm) miongoni mwa michango aliyoitowa kwenye jumuia za chama na chama ni uwezesha wa kiuchumi na kwenye jamii amechangia miundo mbinu mbalimbali ya afya na elimu.
Mbunge Taska
Mbogo amesema katika kipindi hicho ameweza kutembelea
jumla ya Kata ya 53 kati ya Kata 58 zilizopo katika
Mkoa wa Katavi na aliweza kufanya kazi pia ya kuimalisha chama na
kuwaeleza wananchi yale mambo mazuri yaliofanywa na
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Amesema ameweza
kufanikiwa kuwaeleza wanawake wajiunge kwenye
vikundi ili waweze kukopesheka kwani mikopo
kwa ajiri ya akina mama vijana na watu wenye
ulemavu ni swala la kisheria kwa kila Halmashauri zote nchini kutenga
asilimia kumi kwa ajiri ya makundi hayo kutoka kwenye mapato yao ya
ndani .
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa
wa Katavi Idd Kimanta amewapongeza wabunge Taska Mbogo na Matha Mariki kwa kazi yao kubwa ya kuwatumikia wananchi .
Alisema wabunge hao wa viti maalumu wamefanya kazi kubwa ya kutoa michango kwenye jumuia yao na kwenye jumuia nyingine za chama na kwenye jamii.