Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi akichangia hoja mbalimbali bungeni Mjini Dododoma |
Malalamiko ya wanachi hususani wa Manispaa ya Mpanda ya muda mrefu juu ya makinikia ya Madini kwenye eneo Kampuni limepata mwarobaini wake baada ya Serikali kutoa majibu ya swali hilo kufuatia Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi kujibiwa swali lake Bungeni la kuitetea Manispaa ya Mpanda.
Katika swali lake la Bungeni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi ameuliza swali kuwa ‘’Halmashari ya Manispaa ya Mpanda wamekuwa wakihifadhi mchanga wa madini teils kwa muda mrefu cha ajabu waowameambiwa tu watapewa tozo ya huduma kwanini wasipewe asilimia sehemu ya mauzo ya mchanga huo? ‘’amehoji Kapufi
Katika hatua nyingine Mbunge huyo ameuliza awali halmashauri walikuwa wanashiriki biashara ya kokoto kwenye eneo hilo vigezo vilivyotumika kuiruhusu Halmashauri kufanya biashara ya kokoto kwanini isitumike kwenye biashara hiyo ya Tails.
Akijibu Maswali hayo Bungeni Mjini Dodoma Naibu waziri wa Madini Judithi Kapinga amesema jambo hilo linawezekana na kuiomba kuishauri Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kufanya mazungumzo na mmiliki wa mchanga huo kama kuna uwezekano wa kuwa sehemu ya mauzo ya mchanga huo wa marudio.
Kapinga ameeleza kuwa kwa upande wa serikali kupitia wizara ya Madini watafurahi kushiriki kusaidia katika mazungumzo hayo yaweze kufanyika ili kama kunauwezekano Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda iwezekunufaika pia katika masuala hayo ambayo Mbunge ameyasema.Judithi Kapinga
Kwa mara kadhaa kupitia vikao vya baraza la madiwani la Manispaa ya Mpanda madiwani wamekuwa wakihoji juu ya unufaika wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kwakuwa kazi hiyo ya uchimbaji inafanyika kwenye kata ya Misunkumilo iliyopo ndani ya Manispa ya Mpanda.