Na, Jackison Gerald.Katavi.
Viongozi wa dini,wazee wakimila na asasi mbalimbali za
kiraia wameshauliwa kuimarisha ushirikiano wa kupambana na kuzuia vitendo vya
rushwa katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea kufanya uchaguzi mkuu ili
kuisaidia jamii kuwa na uelewa juu ya madhara ya rushwa katika uchaguzi wa viongozi jambo litakalo
saidia kupata viongozi wenye
ueledi na watakao jali haki na uajibikaji katika kuleta maendeleo kwa wananchi..
Akizungumza wakati akifungua semina kwa viongozi wa dini
,wazee wakimila na asasi mbalimbali za kiraia Naibu mkuu wa takukuru Stewart
kiondo amesema ibara ya (9)h ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inaelekeza mamlaka za nchi , taasisi zake na nchi kwa
ujumla kuhakikisha zinaelekezwa ili kuitokomeza rushwa.
Stewart kiondo Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi akitoa mafunzo kwa viongozi wa dini ,wazee wa kimila na asasi mbalimbali za kiraia
Kiondo amesema utekelezaji wa masharti ya katiba kuhusu kutokomeza rushwa umebainishwa katika sheria
ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 na kifungu cha (7)b kikisomwa na
kifungu cha (15) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 kikiitaka takukuru kuhamasisha ushiriki wa wadau ,wananchi ,taasisi na mamlaka mbalimbali
katika kuondoa rushwa nchini.
Ameeleza kuwa kwa upande wa viongozi wa dini hekima na
busara zitumike ili wagombea wasitumie mianya ya ununuzi wa vifaa au uboreshaji wa miundo mbinu ya
nyumba za ibada au kutoa fedha kwa ajili ya kuwavutia wananchi ili wapate fursa
ya kuchaguliwa.
Amewataka kukemea kauli ya unatuachaje pindi mgombea
anapokuwa amepita katika maeneo mbalimbali ili kukabiliana na vitendo
hivyo.
Kaim Katibu tawala Mkoa wa Katavi Florence chrisant
amewasisitiza viongozi wa dini ,wazee wa kimila na asasi mbalimbali za kiraia
kuona umuhimu wa kudhibiti vitendo hivyo kwani vinawanyima haki Watoto wa
maskini wenye ndoto ya kuwa katika nyazifa mbalimbali za uongozi.
Chrisant amewaomba kudumisha amani na mshikamano kuelekea
uchaguzi mkuu ili kuwezesha uchaguzi huru na wahaki utakao saidia kupata
viongozi wenye ueledi na watakao jaiil haki za wananchi.
Kaim Katibu tawala Mkoa wa Katavi akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha mafunzo ya kupambana na kuzuia rushwa kwa viongozi wa dini, wazee wa kimila na asasi mbalimbali za kiraia kilicho fanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Akitoa mafuzo juu ya kukemea vitendo vya rushwa Afsa kutoka
taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa leonard Minja amewaeleza viongozi wa
dini wazee wa kimila na asasi mbalimbali za kiraia kuhamasisha jamii juu ya
kuripoti vitendo vya rushwa ambavyo wenda vikafanywa na wagombea kupitia
majukwaa mbalimbali ya kisiasa ,misiba na vikao mbali katika kipindi hiki
ambacho inchi inaelekea katika uchaguzi.
Minja ameeleza kuwa mpaka sasa takukuru wameisha toa
mafunzo kwa viongozi wa bodaboda na
makukundi mbalimbali kupitia mikutano ya hadhara.
Amewasisitiza viongozi wadini kuona umuhimu wa kupinga rushwa na kuonyesha ushirikiano wa dhati bila kuchoka kama ambavyo wemekuwa hawachoki katika kutoa elimu ya dini na mafundisho mbalimbali ya kumjua mungu.
Viongozi wa dini ,wazee wa kimila na asasi mbalimbali za kiraia wakiwa katika mafuzo ya kuzuia na kupambana na rushwa yatakayo wawezesha kuoa elimu katika majukwaa mbalimba
Amewaeleza kuwa takukuru itakuwa Pamoja na wao katika vita
hii ya kutokomeza vitendo vya rushwa kupitia majukwaa mbalimbali ndani ya Mkoa
huo.
Sheikhe wa Mkoa wa Katavi Mashaka Kakulukulu ameishukuru taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru Mkoa wa Katavi kwa kuwapatia elimu madhehebu ya dini ,wazee maarufu viongozi wa kimara na asasi mbalimbali za kiraia juu ya madhara ya rushwa wakati wa uchaguzi.
Sheikh wa Mkoa wa katavi mashaka kakulukulu ameishukuru taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa takukuru kuona umuhimu wa mafunzo hayo kwa wakati muafaka ambao taifa linakwenda kufanya uchaguzi wa Rais wabunge na madiwani na yeye binafsi mafunzo hayo yamemuongezea uelewa juu ya vitendo hivyo vya rushwa na anakwenda kuwaeleza waumini kuwa chochote watakacho kifanya kutokana na rushwa madhara yake yatakuwa ni yapi .
Kwa umoja wao viongozi wadini, wazee wa kimila na asasi mbalimbali za kiraia wamesema elimu hiyo amewapa uelewa mpanda juu ya mianya ya rushwa na wanakwenda kutumia majukwaa mbalimbali kuwaeleza madhara ya rushwa ili kujenga jamii yenye uadili na inayo tambua madhara ya rushwa.
mwisho.