Amcos za takiwa kuingia mikataba na makampuni yatakayo walipa kwa wakati na yenye ofisi Mkoani Katavi

 Na Muandishi wetu

           Katavi

Wakulima  wa Tumbaku  Mkoani  Katavi  wametakiwa  kutafuta  kampuni za ununuzi wa tumbaku  watakazo ingia nazo mikataba ya kununua tumbaku kampini zenye uwezo wa kiuchumi zitakazo walipa kwa wakati na zenye ofisi zao ndani ya Mkoa wa Katavi

.Wito huo umetolewa na  Mrajisi  msaidizi wa  vyama vya ushirika Mkoa wa Katavi Peter Nyakunga  wakati   akizungumza  na  wakulima wa tumbaku  wa Amcos ya Kasi kwenye mkutano mkuu maalumu  uliofanyika katika kijiji cha ivungwe katika Manispaa ya Mpanda .

 Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Katavi Peter Nyakunga akifafanua namna ya utaratibu wa Amcos juu ya kuingia Mikataba na makampuni ya ununuzi wa tumbaku wakati wa mkutano mkuu maalumu wa Amcos ya Kasi.

Amebainisha kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya Amcos  kuingia  mikataba ya  kuuza  tumbaku   kwenye  makampuni  ambayo   hayana uwezo wa kuwalipa fedha zao wakulima kwa wakati na ambazo hazina  hata ofisi ndani ya Mkoa huo.

Hali hii imekuwa ikiwafanya hata wakulima  wakitaka  kudai haki yao au mambo mengine  mbalimbali yanayohusu zao hilo  inakuwa   kwao sio  rahisi kwa kuwa baadhi ya makampuni walio ingia nayo mikataba ya ununuzi wa Tumbaku  hayana ofisi  katika Mkoa huu wa Katavi .

Nyakunga amesisitiza kuwa Serikali inao wajibu wa kuzisimamia    Amcos    na kulinda masilahi ya wakulima  lakini nao   wakulima    wanayo  haki na wajibu wa kuchagua  kampuni ambayo wanataka kufanya nayo  biashara  hivyo  ni jukumu lao wakulima wenyewe kuchagua kampuni wanayotaka kuingia nayo mkataba.


 

 Wao  kama serikali ni wajibu wao kuwaambia wakulima na kuwashauri  kwa  kuwa huwa wameisha   jua  uwezo wao wa kiuchumi  wa makampuni ambayo yanatakaka kufanya  mikataba

Alitoa  mfamo wa Kampuni ya MAGEFA ambayo   inalalamikiwa na Amcos ya Kasi  kwa kuchelewa  kuwalipa wakulima wa Amcos  hiyo kiasi cha  dola za Kimarekani 313,261.05  wao  kama  mkoa waliwashauri wakulima  kwenye mkutano juu ya  kutoingia mikataba   na  makampuni yasiyo na ofisi kwenye Mkoa huu lakini wakulima waligoma  na sasa wamerudi kwao kuomba kuwasaidia na wao  kwa kuwa wakulima wote ni wao  wanafanya  jitihada  za kuhakikisha wakulima wanalipwa  madai yao .

Amefafanua kuwa  sio kwamba ni Serikali ya Mkoa tu  inayofatilia  madai hayo ya wakulima hao  ni   mpaka Waziri wa Kilimo anajua  na ndio maana anafuatilia   kwa karibu sana  kwa  kuwa anatambua  kulitokea changamoto ya makampuni mengi kununua tumbaku nje ya  yale makisio yao .

Mkulima Cristopher Januari  alimuomba  mrajisi  msaidizi  aendelee kuwasaidia kama ambavyo amekuwa akiwasaidia kwa kuwa yeye ndie mlezi wao na baba yao wa Amcos zote katika Mkoa wa Katavi na pia aendelee kufuatilia walipwe fedha wanazo dai.



Mwenyekiti wa Amcos ya Kasi Deis Maganga amesema Mrajisi  msaidizi  amekuwa bega kwa bega na wakulima  hata wanapokuwa kwenye changamoto amekuwa nao na ndio maana hata hivi karibuni alikwenda kufuatilia madai yao ya fedha za wakulima wanazo dai .

Maganga amesema mrajisi msaidizi wa mkoa wa Katavi wakulima wote ni wake na  watoto wake hivyo  wanapokuwa wamekosea awasamehe kwani wamekuwa wakitoa mambo yao nje kabla ya wao kuwa wamekaa  hivyo ni sawa na wao kudai haki bila kufuata sheria.




 Baadhi ya wakulima wa Kasi Amcos wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatilia kwa makini 


MWISHO

 

 

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages