| Jonh Mwaipungu mrakibu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi na Afisa Polisi Jamii mkoa wa Katavi akitoa elimu kwa vikundi vya Polisi Jamii Wilaya ya Mpanda |
Na Paul Mathias-Katavi
Vikundi vya ulinzi shirikishi katika Manispaa ya Mpanda wamepatiwa semina maalumu ya namna bora ya kutimiza majukumu yao kwenye kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
| Baadhi ya Polisi Kata Wilaya ya Mpanda wakiwa kwenye semina hiyo ya masuala ya ulinzi shirikishi |
Vikundi vya ulinzi shirikishi katika Manispaa ya Mpanda wamepatiwa semina maalumu ya namna bora ya kutimiza majukumu yao kwenye kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Semina hiyo imetolewa na Jonh
Mwaipungu Mrakibu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi na afisa polisi jamii mkoa
wa Katavi amesema kuwa lengo la semina hiyo ni kuwambusha polisi kata na
vikundi vya ulinzi shirikishi kwenye kata zao kuwajibika kwa kuzingatia
taratibu na kanuni.
Ameeleza kuwa dhana ya ulinzi shirikishi imekuwa na matokeo mazuri kwenye jamii kwakuwa wananchi wamekuwa na uwezo wa kutoa taarifa za wahalifu na wahalifu kuanzia ngazi ya jamii kupitia falsafa ya polisi Jamii.
Mwaipungu amesema kuwa dhana ya
polisi jamii imekuwa na tija kwa jeshi hilo kwa kutoa wigo mpana kuwa karibu na
jeshi la polisi kwa kuwa sehemu ya kulinda Amani kupitia vikundi vya ulinzi
shirikishi.
Amebainisha kuwa katika kuhakikisha vikundi vya ulinzi vinakuwa hai kwa kuendelea kutoa elimu na kuvihuisha vikundi zaidi kwa lengo likiwa ni ktokomeza uhalifu kwenye jamii.
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa
vikundi shrikishi wamesema semina hiyo itakwenda kuongeza uwajibikaji kwa
kufanya kazi zao kwa kuzingatia taratibu na sharia zilizopo.