![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko [katikati]akitoa maelekezo ya ujenzi wa Daraja la Katuma eneo la sitalike alipotembelea na kujionea mwenendo wa ujenzi huo. |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amemshukuru Rais Dk
Samia Suluhu Hassan kwa jitihada
kubwa sana za kuhakikisha kwamba katika kipindi chake cha utawala anaondoa changamoto mbalimbali za
barabara zinazouunganisha Mkoa wa Katavi na Mikoa mingine na barabara za
ndani ya mkoa.
![]() |
| Muonekano wa Daraja la Katuma sitalike linalounganisha Mkoa wa Katavi na Rukwa ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 83% |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amemshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa sana za kuhakikisha kwamba katika kipindi chake cha utawala anaondoa changamoto mbalimbali za barabara zinazouunganisha Mkoa wa Katavi na Mikoa mingine na barabara za ndani ya mkoa
Pongezi hizo amezitowa wakati alipokuwa akikagua
utekelezaji wa ujenzi wa Daraja
la Sitalike lenye utefu wa Mita 55 linalojengwa kwa
Zaidi ya Bilioni 9.1
linalouunganisha Mkoa wa Katavi na Mkoa wa Rukwa pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Katavi
ambalo limekuwa na changamoto ya muda
mrefu wakati wa kipindi cha masika
Mrindoko amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa katika kipindi cha uongozi wake kuhakikisha anaondoa miundo mbinu mbali ya barabara inayouunganisha Mkoa wa Katavi na Mikoa mingine .
Amebainisha kuwa tunafahamu
kuwa mkoa huu umetoka mbali katika
maswala ya upatikanaji wa
barabara kuu na wanaendelea kwa kasi
kubwa sana kwa ujenzi wa barabara zito
zinazounganusha mkoa huu na mikoa mingine
kuwa zinapitika katika kipindi chote cha mwaka mzima .
Ameeleza kuwa daraja hilo lilikuwa na adha kubwa hasa wakati wa kipindi cha mvua kama ambazo zilitokea hivi karibuni mwaka 2024 wananchi walikwama na kulazimika kulala porini ndani ya hifadhi ya Katavi baada ya daraja sasa kufunikwa na maji kwa muda wa siku kumi na nane,(18)
Mrindoko amefafanua kuwa ndio maana ametoa shukurani kwa
Rais Samia ametowa fedha kwa kupitia Benki ya Dunia kwa lengo la kuhakikisha daraja la uhakika zaidi linapatikana katika barabara hiyo muhimu.
Adha
amemshukuru mkandarasi kampuni ya M/S Mselem Civil Engineering
and Buildimg Contractors Limited JV
Mbuyas Contractors Company Limeted kwa kazi walioifanya ya ujenzi wa baraja hilo hali
ambayo inaonyesha litakamilika muda si mrefu na litaanza kitumika .
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Katavi Mwandisi Martin Mwakabende amesema ujenzi wa daraja hilo ni utekelezaji wa ahadi za Rais.
Ambapo ujenzi huo unagharimu kiasi cha Shilingi 9,106,238,961.00 na kazi za ujenzi zinaendelea utekelezaji wake hadi sasa imefikia asilimia 83 huku muda wa utekelezaji ukiwa umefikia muda wa miezi 11 kati ya miezi 12.
Mkurugenzi wa Kampuni ya M/S Mselemu Civil Engineering Nassor Mselemu amesema wanatalajia kukamilisha ujenzi kwa muda uliopangwa licha ya wao kuwa wameomba waongezewe mwezi mmoja wa muda wa ziada.




