WAKULIMA WA TUMBAKU WAPONGEZWA KWA KUJENGA OFISI YA KISASA.

 

Baadhi ya wakulima wa Ivungwe Amcos wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa 6 wa Chama hicho ambao umeambatana na uzinduzi wa ofisi ya kisasa.


Na Mwamdishi wetu

Vyama vya Ushirika nchini vimetakiwa kujiendesha kupitia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuongeza ufanisi, uwazi na uwajibikaji zaidi kwa watumishi wa vyama hivyo wakati wa kuhudumia wakulima.

Vyama vya Ushirika nchini vimetakiwa kujiendesha kupitia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuongeza ufanisi, uwazi na uwajibikaji zaidi kwa watumishi wa vyama hivyo wakati wa kuhudumia wakulima.

Hatua hiyo imesisitizwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini kufuatia kuwepo kwa vikwazo na kudolola kwa uwazi na wajibikaji kwa baadhi ya watumishi wa vyama vya ushirika, jambo ambalo linashusha kasi ya maendeleo ya wakulima wa mazao ya ushirika kama vile tumbaku.

Naibu Mrajis Udhibiti wa Vyama Vya Ushirika Taifa Collins Nyakunga, akifungua jengo la Chama Cha Ushirika Ivungwe Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi jana alisisitiza matumizi ya TEHAMA kwani pia yatarahisisha utendaji kazi.

“Tuhakikishe vyama vinajiendesha kwa kutumia TEHAMA kwa maana ya mfumo utakao rahisisha shughuli zenu kwenye utumaji wa taarifa na ukichelewesha kitu kinaonekana kipo kwako kimekaa muda mrefu, kuweka na kutuza kumbukumbu lakini inapunguza gharama” amesema Nyakunga.

Katika hatua nyingine baada ya kuzindua Jengo la Ofisi Chama Cha Ushirika Ivungwe amewapongeza viongozi wa chama hicho kwani jingo hilo limejengwa kwa ubora na thamani ya ndogo na kuonyesha viongozi wanauadirifu mkubwa.

“Mmetafuta mafudi wenu local fundi ambapo gharama yao sio kubwa ikilinganishwa na ile ya mafundi wa makampuni ya ujenzi…ni wazi hapa kuna jambo kubwa la kujifunza kwamba tunapofanya uwekezaji ni vizuri tutengeneze kitu bora lakini tuangalie kwa jitihada kwa namna yoyote ile tupate jengo lililobora na kwa gharama ndogo” ameeleza Nyakunga.

Katika hatua nyingine amewapongeza wakulima wa Amcos hiyo kwa kuendelea kuzalisha tumbaku yenye ubora na kufanya vizuri katika masuala ya utawala.

“ Ivungwe sasa mnajengo zuri, sasa endeleeni kuzingatia kilimo bora kutokana na miongozo inayotolewa lakini hakikisheni mnaendelea kuwalipa wanachama wenu pesa kwa wakati, mnalipa madeni benki kwa wakati na muanze kuangalia ni kwa namna gani mnaongeza vyanzo vya mapato”

Mrajisi Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Katavi Peter Nyakunga amesema Ivungwe AMCOS katika vyama 53 kuna vyama 25 vimeshiriki kilimo cha Tumbaku kwa msimu wa kilimo 2024/25 na kuna vyama 25 vilishiriki kilimo msimu wa kilimo 2023/24 na kuna vyama sita vimelipa fedha wakulima wake kwa asilimia 100.

Katika vyama hivyo sita Ivungwe AMCOS licha ya kulipa fedha wakulima wake kwa asilimia 100 pia ilifanikiwa kulipa fedha kwa kiwango kilekile cha fedha ambacho kimeingizwa benk na kampuni ya ununuzi na kukabidhiwa mkulima bila makato yoyote, jambo ambalo chama hicho kinatofautiana na vyama vingine vya ushirika mkoani humo.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa ofisi, Meneja wa Ivungwe AMCOS Karoli Nzanza alisema ujenzi huo umegharimu kiasi cha fedha milioni 54 kutoka chanzo cha mapato ya ndani.

Amebainisha kuwa  malengo ya chama hicho cha ushirika yalikuwa ni kujenga ofisi ya kisasa ili kuboresha utendaji kazi kwa kutoa huduma bora kwa wakulima, hivyo fedha zote walizokusanya waliepuka kugawana posho ya vikao mbalimbali ili kutimiza lengo la ujenzi wa ofisi hiyo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages