BODA BODA WASIO NA USAJILI WAONYWA KUJIHUSISHA NA UHARIFU.

Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoa wa Katavi Issack Joseph akizungumnza na waandishi wa habari 

Na Abdi Lunyamila-Katavi

Mwenyekiti wa bodaboda Mkoa wa Katavi Isaack Joseph amewataka Madreva kuwasajili bodaboda waliopo kwenye vituo vyao mbalimbali ili kuepuka vitendo vya uharifu vinavyofanywa na baadhi ya watu ambao siyo Madreva bodaboda.

Mwenyekiti wa bodaboda Mkoa wa Katavi Isaack Joseph amewataka Madreva kuwasajili bodaboda waliopo kwenye vituo vyao mbalimbali ili kuepuka vitendo vya uharifu vinavyofanywa na baadhi ya watu ambao siyo Madreva bodaboda.

Akizungumza na Waandishi wa habari Joseph amesema kuwa hivi karibuni pamekuwa na baadhi ya waendesha pikpiki ambao hujivisha taswira za dereva bodaboda na kufanya uharifu huku wakijitambulisha kuwa bodaboda huku wakiwa hawana usajili Rasmi.

’’ sisi kama viongozi wa bodaboda Mkoa wa Katavi,tunataka viongozi wote wa Kanda zote zinazounda Mkoa wetu wa Katavi kuhakikisha kuwa bodaboda wote wanaopokelewa katika vituo hivyo wawe na nyaraka zote za kuwatambulisha yaani kutika serikali za Mitaa pamoja na nyaraka kutoka katika uongozi wa bodaboda mkoa’’amesema Joseph

 Aidha mwenyekiti huyo amesema kuwa wao kama bodaboda wataendelea kuwa mabalozi wa kuhubiri umoja amani na mshikamano kwa wananchi wa mkoa wa Katavi.

Jouachimu Ndile Mwendesha bodaboda Mkoa wa Katavi amesema wataendelea kutoa taarifa kwa baadhi ya bodaboda ambao wamekuwa na tabia ya kuingia kwenye kazi hiyo pasipo kufuata utaratibu na kujihusisha na vitendo vya uharifu.

“Kwakweli alicho kisema mwenyekiti wetu ni cha msingi na cha kuzingatia ni jambo la msingi kuwatambua wote wanaofanya kazi hii kwani kuna wengine malengo yao siyo mazuri ni kutuchafua sisi wengine ambao hatujihusishi na uharifu’’amesema Ndile

Uongozi wa Bodaboda umeahidi kuhakikisha unashirikiana vyema na serikali ili kuhakikisha amani iliyopo mkoa wa Katavi na Taifa zima kwa ujumla inaendelea kudumu kwani bila amani basi hakuna maendeleo yoyote yatakayofanyika.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages