MWENYEKITI NSIMBO UBOVU WA MAGARI UNAKWAMISHA UFUATILIAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.



Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi,Hewala Malendeja(aliyesimama) akiwa kwenye baraza la madiwani
Na Mwandishi Wetu KTPC,Nsimbo.     

Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi inakabiliwa na ubovu wa baadhi ya magari ambao unasababisha kukwamisha zoezi la ufuatiliaji wa shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo kwa wakati.

Helawa Malendeja ambaye ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo amebainisha hayo jana  wakati akiahirisha kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Mwenyejiti huyo ameweka wazi kuwa anashangazwa na ubovu wa magari uliojitokeza kwa nyakati za hivi karibuni ikiwa ni jambo ambalo hapo awali halikujitokeza,kwani hata pale ubovu wa magari ulipojitokeza yalitengenezwa kwa wakati sahihi.

Ameeleza kuwa kutokana na ubovu huo wa magari imemlazimu hata yeye binafsi kutumia gari lililobovu ambapo inamlazimu kuchelewa kwenye shughuli za miradi ya maendeleo hata ofisini kwake kutokana na kumharibikia awapo njiani.

Kutokana na ubovu huo amezitaka mamlaka husika kutumia mfumo wa zamani wa kutengeneza magari kwani hapakuwa na ucheleweshaji wa matengenezo wa magari ya umma huku akisisitiza kutumia mawakala wa kutengeza magari kama kunaucheleweshaji wowote ule unaojitiokeza kupitia TAMESA.

Scholastica Njovu,Kaim afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya nsimbo mkoa wa Katavi amesema kuwa pamoja na utekelezaji wake wa bajeti zilizopita tangu halmashauri hiyo kuanzishawa mwaka 2013/14 akili bado inakabiliwa na changamoto za  ukosefu wa magari ya kutosha pamoja na ubovu.

Amebainisha kuwa changamoto zingine  ni ukosefu wa nyumba za watumishi ambapo hiyo ni kutokana na fedha kidogo zinatolewa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo,Watumishi kutolipwa stahiki  zao na hivyo kusababisha madeni.

Uhaba wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo,wananchi wanaibua miradi/vipaombele vyao lakini vinashindikana kutekelezwa kwa wakati kwa sababu ya uhaba wa fedha hali ambayo inawakatisha tamaa pia wananchi kutoshindwa kuchangia asilimia ishirini.

Katika namna ya kutatua changamoto hizo Scholastica alisema halmashauri inafanya mategenezo ya magari yaliyopo japokuwa ni machakavu sana na kutenga kwenye makisio ya bajeti ya mwaka 2021/22.

Kwenye bajeti ya mwaka 2021/22 halmashauri imetenga fedha za kununua gari aina ya Pick Double Cabin moja ambapo pia halmashauri inatarajia kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi mtendaji kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Vilevile halmashauri hiyo imetenga bajeti kwa ajili ya kupunguza madeni ya watumishi katika bajeti ya mwaka wa fedha sambamaba na kuendelea kuomba fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo kutoka serikali kuu.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages