ZAIDI YA TRILIONI 1.93 ZA TENGWA KUBADILI SEKTA YA MIFUGO NCHINI


Katibu Mkuu wa Mifugo Tixon Nzunda


 Na Neema Hussein, Katavi

Wataalam wa Mifungo na Uvivu kutoka Kanda ya nyanda za juu kusini na Magharibi, wameiomba serikali  kuruhusu maeneo ya TFS kulishia Mifugo hasa kwa kipindi kigumu cha kukosa malisho ili kuepusha kuipoteza Mifugo hiyo kwa kukosa chakula.

Hayo yamesemwa na Daktari wa Mifugo kutoka Mkoa wa Mbeya Samora Mshang'a, wakati akiwasilisha changamoto zinazowakabili wataalamu hao katika kikao cha siku mbili kilicho fanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Samora amewasilisha changamoto hizo  mbele ya Katibu Mkuu wa Mifugo Tixon Nzunda, kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,mbali na malisho pia wameomba Wizara hiyo iwe inafanya rejea ya mara kwa mara kuhusu bei elekezi ya uuzaji wa Mifugo ili iwe inaendana na bei ya soko.

Wataalam hao wamesema Mifugo inahitaji chakula hivyo  kuna wakati maeneo yaliyotengwa kwaajili ya malisho yanaishiwa kabisa chakula licha ya wafugaji kuyaendeleza maeneo yaliyotengwa kwa kupanda malisho hayo.

"Kutokana na tukio lililotokea mwaka uliopita la ukame mkali inabidi tuangalie maeneo hayo kama itawezekana lakini pia tunaswala la chanjo za Mifugo bei ya chanjo bado iko juu sana tunaomba Wizara iliangalie hili hasa tukiangalia chanjo ya kichaa cha mbwa," alisema Samora.

Akijibu changamoto hizo  Katibu Mkuu wa Mifugo Tixon Nzunda amesema majawabu ya changamoto hizo wanayo wenyewe na wanaweza kuzigeuza changamoto hizo kuwa fursa.

Nzunda amesema wanataka kuhakikisha Mifugo yote inatambuliwa na inaingizwa kwenye mfumo hiyo itasaidia kutambua idadi ya Mifugo ili waweze kuihudumia.

"Utambuzi wa mifugo sio siasa ni Jambo la kiutendaji, duniani kote swala la utambuzi nilalazima na faida zake zinajulikana maswala ambayo niyamsingi hayawezi kuwa ya kujadiliana kwa karne hii ya 2022 na yeyote anaye tuchelewesha hatutamuacha,"alisema Katibu Mkuu Nzunda.

Amesema vyama vya wafugaji, Watendaji wa sekta ya Mifugo, Viongozi wa mamlaka za serikali za mitaa na Mikoa lazima wahakikishe Jambo hilo la utambuzi wa mifugo linafanyika na linafanyika kwa weledi ikiwemo kulipa msukumo wa kipekee.

Amesema swala la kuruhusu mifugo kuingizwa kwenye hifadhi za Taifa kwaajili ya maoisho haliwezi kuwa Jambo la kujivunia na suluhisho la kudumu la malisho ni kuwa na mashamba ya malisho kwa wafugaji nakusema kuwa wao ni nchi moja hivyo mifugo wanaihitaji na Hifadhi zinahitajika kwaajili ya Watalii.

Nzunda amesema hawawezi kujenga sehemu moja huku sehemu ya pili wanabomoa kwani mfumo wa nchi unaongozwa na katiba,sheria,kanuni na taratibu hivyo taratibu hizo lazima ziheshimiwe na zifuatwe.

Katibu Nzunda amesema mtizamo wake na mtizamo wa Rais Samia ni kufanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya Mifugo na tayari wameandaa mpango  mkakati wa miaka mitano utakao gharimu rasilimari zaidi ya Tirion 1.93  kwaajili ya kubadilisha sekta ya Mifugo.

Amesema wamechoka kuwa na mifugo isiyokuwa na tija na kutochangia pato la Taifa na kuongeza kuwa ni lazima waanze kubadili mfumo wa fikra za wafugaji wajione ni wawekezaji na kuondokana na Ufugaji wa uswagaji kwenda kuwa wafugaji.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages