Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi,Faustine Maijo akitoa taarifa leo mapema kwa waandishi wa habari ya utekelezaji wa kazi wa taasisi hiyo ya robo mwaka. |
Na George Mwigulu,Katavi.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Mkoa wa Katavi imebaini kuwepo kwa mapungufu mbalimbali yakiwemo usimamizi mbovu ujenzi miradi,ukiukwaji wa mikataba na ucheleweshaji wa kukamilisha miradi mitano katika halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Mkoani hapa.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi wakiwa kwenye majukumu ya kutekeleza kazi leo mapema katika ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Katavi.Picha na Paul Mathias.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Mkoa wa Katavi imebaini kuwepo kwa mapungufu mbalimbali yakiwemo usimamizi mbovu ujenzi miradi,ukiukwaji wa mikataba na ucheleweshaji wa kukamilisha miradi mitano katika halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Mkoani hapa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi,Faustine Maijo ofsini kwake wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ya utekelezaji wa kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha mienzi mitatu kuanzia January hadi March mwaka huu.
Maijo amebainisha kwa kipindi cha robo ya mwaka wameweza kufuatilia miradi tisa yenye thamani ya Bil 1.591 kwenye sekta ya ujenzi,elimu na afya ambapo miradi miwili imekamilika huku miradi miwili ikiendelea vizuri na miradi mitano imekutwa na mapugufu.
Miradi iliyokutwa na mapugufu hayo ni pamoja na ujenzi wa vyumba za walimu shule ya Msingi Lwega katika halmashauri ya wilaya ya Tanganyika wenye thamani ya Mil 97 ambapo uchuguzi umebaini kuwa kunaukiukwaji wa taratibu za mkataba na kujenga kinyume na kiwango ilivyoainishwa kwenye mkataba.
‘’…tumebaini vilevile mapugufu katika ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Lwega wenye thamani ya mil 64 ambapo ndugu wanahabari thamani ya mradi hauedani na fedha halisi (VALUE OF MONEY) iliyotolewa na serikali '' amesema Maijo.
Ujenzi wa mradi mwingine umekutwa na madudu ni
ujenzi wa kituo cha afya cha Kata ya Karema Wilaya ya Tanganyiga wenye thamani
ya Mil 100 ambapo uchuguzi umebaini kuwa kuna ucheleweshwa we fedha.
Mkuu wa TAKUKURU huyo amesema wamebaini mapugufu katika ujenzi wa mabweni na maabara katika shule ya sekondari Kakoso Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika wenye jumla ya thamani ya Mil 300 ambapo kwenye ujenzi wa mabweni wamebaini usimamizi mbovu,ucheleweshwaji wa fedha na mradi wa maabara kumekuwa na ukiukwaji wa taratibu za mkataba kwa kujenga chini ya kiwango.
Aidha amebainisha kuwa TAKUKURU imeendelea kufanya chambuzi za mifumo ikiwa na lengo la kubaini mianya ya rushwa ambayo inaweza kupelekea vitendo vya rushwa na kushauri Taasisi husika kuona namna bora ya kurekebisha mapungufu yaliyobainika kwenye mifumo.
Vilevile amewataka wananchi wa Mkoa wa Katavi kuendelea kutoa taarifa mara moja pindi wanapobaini kuna viashiria vya rushwa kwenye maeneo yao kwani TAKUKURU iko tayari kutoa ushirikiano wa kuhakikisha wahusika wanakamatwa.