Baadhi ya meno ya Tembo yaliyokamatwa na jeshi la polisi katika mkoa wa katavi |
Na Walter Mguluchuma, Katavi .
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Askari wa Hifadhi ya
Taifa ya Katavi wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne
wakiwa na meno ya Tembo vipande 16 ambavyo ni sawa na tembo saba
hai katika matukio mawili tofauti .
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne wakiwa na meno ya Tembo vipande 16 ambavyo ni sawa na tembo saba hai katika matukio mawili tofauti .
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Katavi Kaster Ngonyani ameeleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa kufatia
msako mkali uliofanywa na Askari wa jeshi la polisi kwa
kushilikiana na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi mara baada ya kuwa
wamepata taarifa juu ya watu hao kujihusisha na biashara halamu ya nyara
za serikali.
Katika tukio la kwanza lilitokea katika maeneo
ya Mtaa wa Kwalakwacha Kata ya Nsemlwa Manispaa ya Mpanda
mtuhumiwa Juma Malongo (47) Mkazi wa Mtaa wa Kozazi Manispaa
ya Mpanda alikamatwa akiwa na vipande kumi vya meno ya tembo
Mtuhumiwa huyo alikuwa ameficha meno ya
tembo katika chumba alichokuwa akiishi kwa kwenye
mfuko wa salifeti .
Kaimu Kamanda Ngonyani amesema tukio
jingine lilitokea huko maeneo ya Itunya Tarafa ya
Kapalamsenga Wilaya ya Tanganyika ambapo watuhumiwa
watatu ambao Edesi Maridadi (62) mkazi wa Kalia
Kabwe Wilaya ya Nkasi Riukwa , Silas Maiko(19) na
Julius Msumeno wakazi wa Kalia Kabwe walikamatwa wakiwa
na vipande sita vya mano ya tembo .
Amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na nyara hizo za
serikali wakiwa wamehifadhi ndani ya nyumba yao waliyokuwa wakiishi kwa lengo
la kutafuta mteja ili waweze kufanya biashara haramu.
Aidha katika eneo la Kaburiwazi ndani ya
pori la akiba Rukwa wilaya ya Mlele Mkoa wa
Katavi wamekamatwa watuhumiwa watano wakiwa na silaha aina ya
Gobole mbili pamoja na nyama ya pori.
Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Pius Mbalamwezi
Edward John , Good frey Mwaka ,Crispin George na Gelad
Mashamba wote wa kazi wa Kijiji cha Muze Wilaya ya
Sumbawanga Mkoani Rukwa .
Mhifadhi Mwandamizi, Kaimu Mhifadhi ya Hifadhi ya
Taifa ya Katavi Francis Kone Makaranja amesema
kuwa wanyama hao wamekuwa wakiuawa kwenye maeneo ya nje ya Hifadhi ya
Taifa ya Katavi.
Amefafanua kuwa wamekuwa wakileta nyara hizo za serikali
kwa lengo la kuja kuzificha na kutafuta soko lakini kutokana na ushirikiano
mkubwa wa vyombo vya ulinzi na usalama vinavyoshirikiana na askari wa
Hifadhi ya Katavi wameweza kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao .
Makaranja amewaonya watu wote ambao wanajihusisha na
swala la ujangili waache mara moja kwani watumbue kuwa
ulinzi ulipo ndani na nje ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi ni kubwa
Watuhumiwa hao bado wanaendelea kuhojiwa na mara uchunguzi utakapokuwa umekamilika watafikishwa mahakamani ili wakajibu tuhuma zinazo wakabili .