Na Paul Mathias,Mpanda.
Wananchi katika Kijiji cha
Kanoge Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamesema kuwa serikali kupitia Wakala wa
Maji na usafi wa Mazingira Vijijini Ruwasa Wilaya ya Mpanda Kuja na Mfumo wa kulipia
huduma ya Maji kwa Luku utasaidia ukusanyaji wa Mapato kwa serikali.
Moja ya Mita ya Maji iliyofungwa katika mfumo wa luku katika kijiji cha Kanoge ambapo wananchi watalipia huduma ya Maji katika mfumo wa Luku kadri ya mahitaji yao |
Wananchi katika Kijiji cha Kanoge Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamesema kuwa serikali kupitia Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini Ruwasa Wilaya ya Mpanda Kuja na Mfumo wa kulipia huduma ya Maji kwa Luku utasaidia ukusanyaji wa Mapato kwa serikali.
Wananchi hao wamebainisha hayo
kijijini hapo Baada ya kufikiwa na chombo hiki ili kufahamu namna mfumo huu
utawasaidia wananchi na serikali katika kupata kukusanya mapato na huduma ya
maji kijijini hapo.
Akisa Linus Mkazi wa kijiji cha
Kanoge amesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuja na Mfumo wa kulipia Maji kwa
njia ya Kadi ambayo itaepusha usumbufu wa upatikanaji wa huduma ya maji na
kusaidia Mapato ya serikali.
Wakazi wa Kijiji cha Kanoge wakiendelea kupata huduma ya Maji kupitia mfumo wa lipa kabla ambao ambao umeletwa na Ruwasa kwa lengo la kukusanya mapato na kuepusha upotevu wa Maji |
Kwa upande wake Abikolimana
Yusuph Mkazi wa kijiji cha Kanoge amesema Mara baada ya Serikali kuleta Mradi
huo kupitia Ruwasa baada ya muda walileta Mfumo wa kisasa wa kulipia huduma ya
Maji kupitia kadi kwa mfumo wa Vocha.
‘’Abilikomama anasema unaweka
Pesa kwenye ile kadi halafu ndo unaenda kununua kulipia maji pale ukiweka kadi
hiyo kwenye Mita Maji yanatokana kulingana na kiwango ulicholipia’’
Elisha Chagula mwenyekiti wa Kamati
za Watumiamaji katika Kijiji cha Kanoge na Litapunga ameiomba serikali
kuendelea kuweka mifumo hiyo kwenye maeneo mengine kwakuwa ni lafiki kwa
Mwanachi na unaisadia serikali ukusanyaji wa Mapato.
Kaimu Meneja wakala wa maji na
usafi wa Mazingira Ruwasa Wilaya ya Mpanda Mhandisi Christian Mpena amesema
Wilaya ya Mpanda imepokea mita za luku za maji tatu ambazo zimefungwa katika
Kijiji cha Kanoge Sokoni,Kituo cha afya Kanoge na Shule ya Msingi Stalike.
‘’natoa shukurani za pekee kwa
serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa Mpanda tulipokea [Water miter Pre
Paid] mita za luku za maji tatu ambazo zimefungwa shule ya msingi Stalike,Kituo
cha afya kanoge na kijiji cha Kanoge sokoni’’amesema Mpenda.
Moja ya Mita ya maji iliyofungwa katika Kituo cha Afya Kanoge ambayo inatumia Mfumo wa Luku kwa watuamiji wa Maji kulipia kabla ya kupata huduma hiyo |
Katika hatua nyingine ameawaomba wananchi kuendelea kuitunza miundo mbinu hiyo ambayo inaletwa na serikali kwenye maeneo yao.