| Baadhi ya Wakulima wa Kasi Amcos wakiendelea na shuhguli za kilimo cha Tumbaku. |
Na Mwandishi wetu-Katavi
Wakulima wa zao la Tumbaku wa Amcos ya KASI katika Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wameishukuru Bodi ya Tumbaku Tanzania kwa kuwasaidia kuweza kulipwa fedha zao Zaidi ya Dolla 312,000 ambazo walikuwa wanadai mrefu kutoka kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya Magefa.
Wakulima wa zao la Tumbaku wa Amcos ya KASI katika Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wameishukuru Bodi ya Tumbaku Tanzania kwa kuwasaidia kuweza kulipwa fedha zao Zaidi ya Dolla 312,000 ambazo walikuwa wanadai mrefu kutoka kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya MagefaWakizungumnza na Gazeti hili wakulima
hao wameeleza kuwa kilio cha kutolipwa fedha zao za msimu wa Tumbaku
uliomalizika mwaka huu kilikuwa cha muda mrefu tangu walipo maliza masoko yao
mwezi wa Julai.
Lameck Mbuza Mkulima wa Kasi Amcos amesema
wao kama wakulima wamepitia kipindi kigumu kabla ya malipo hayo kufanyika
walikuwa wameingika madeni mitaani lakini baada ya malipo kufanyika wameweza
kurejesha.
lameck Mbuza Mkulima wa Kasi Amcos akielezea namna malipo yao ya Tumbaku yalivyosaidia kubadilisha maisha yao.
Hali hiyo imewafanya waendelee na shughuli za
kilimo cha Tumbaku kwa msimu huu kwani pembejeo zote zipo za kutosha na
zimefika kwa wakati kwa hiyo
watahakikisha wanalima kwa nguvu.
‘’tunamshukuru Mkurugenzi wa bodi ya
Tumbaku Tanzania kwa kufika mkoa wa Katavi pindi tulipokua tunadai tunaamini
kufika kwake kumeleta msukumo wa kufanyika kwa malipo yetu yaliyokua
yamekwama’’ amesema Mbuza.
Ameyaomba Makampuni yanayoingia
mkataba wa ununuzi wa Tumbaku kwenye vyama vya msingi kuharakisha malipo pindi
wamapo kuawamenunua Tumbaku ya wakulima na kuwafanya wakulima kuwa na ari ya
kulima kwani nao wanatamani kutembelea Magari na kuishi maisha mazuri yenye
uchumi imara.Gerald Kipanta Makamu mwenyekiti wa Kasi amcos akiishukuru serikali kwa kuwalipa fedha zao Tumbaku.
Paul Yahila Mkulima wa Kasi Amcos
ametoa ushauri kwa makampuni ya ununuzi
wa Tumbaku kufata sheria na taratinu ili kuepusha kuwepo kwa changanoto
ya wakulima kucheleweshewa malipo yao.
Amebainisha kuwa kilimo cha Tumbaku wanakianza
mwezi Agosti lakini changamoto inatokea pale malipo yanapochelewa huwa wanaumia
sana hali ambayo huwapelekea kwenda mitaani na kuchukua mikopo isiyorasmi
ambayo hua na riba kubwa.
‘’Msimu huu tumelipwa mwezi huu wa Novemba na tulianza maandalizi ya kilimo mwezi wa Agosti hali hii hua inawavunja nguvu wakulima’’amesema Yahila.
Joseph Yamala amesema kabla ya malipo
ya Tumbaku walipitia maisha magumu kwenye kuendesha maisha yao huku akishukuru
baada ya malipo mambo yamekaa sawa na wanaendesha maisha yao kama kawaida.
Katika hatua nyingine amewashukuru
viongozi wa Chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Katavi Latcu na Mlajisi Msaidizi
Peter Nyakunga kwa jitihada mbalimbali walizozifanya.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa
Kasi Amcos Gerald Kipanta ametoa shukrani za pekee mkurugenzi wa Bodi ya
Tumbaku Tanzania kwa msukumo mkubwa alioufanya mpaka wakulima wamelipwa fedha
zao na sasa wengine wanenunua viwanja ,Bajaji,Pikipiki na wengine wanasomesha
watoto wao waliokuwa wamekwama kuwapeleka shule kwa kukosa pesa.
Kipanta amesema wakulima wao wote wamelipwa fedha zao Zaidi ya Dolla 312,000 ambayo ni malipo ya zao hilo kwa wakulima kwa msimu wa kilimo wa 2024/2025.
Stanley Mnozya Mkurugenzi wa Bodi ya
Tumbaku Tanzania ameagiza makampuni yote yanayonunua Tumbaku kuhakikisha
wanafanya malipo ya wakulima kwa muda muafaka kwa mujibu wa sharia.
Mnozya ameeleza kuwa kwa sasa katika
mkoa wa Katavi wakulima wote wa zao hilo wamelipwa fedha zao kiasi cha zaidi ya
Dolla Milioni 47 sawa na Zaidi ya Bilioni 120 hivyo kwa sasa hakuna wakulima
kwa mkoa wa Katavi wanaodai fedha za msimu uliopita.
Amebainisha kuwa alipokuwa Mkoa wa Katavi alikutana na malalamiko ya wakulima wa chama cha ushirika cha Kasi na kuwaahidi kwenda kufatilia changamoto yao ambayo aliishughulikia na wakulima wamelipwa fedha yao waliokuwa wanadai.